PAMOJA na
kufungwa mabao 2-1 na Mali, timu ya taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri
chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes bado inaweza kusonga mbele katika kufuzu
kwa mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa umri huo, Afcon endapo itachanga vizuri
karata zao katika mchezo wa marudiano.
Baada ya
kufungwa 2-1 katika mchezo wa kwanza wa raundi ya pili wa kufuzu kwa Afcon leo kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Ngorongoro Heroes sasa inahitaji
ushindi wa angalau mabao 2-0 ili kusonga mbele.
Timu hiyo
iliitoa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa penalti 6-5 baada ya kutoka suluhu
katika mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaama na baadae kupata matokeo kama
hayo nchini Congo kabla ya kwenda katika matuta.
Mchezo huo
uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, umeifanya Ngorongoro kuwa na
kibarua kigumu katika mchezo wa marudiano kwani sasa inahitaji ushindi wa
kuanzia mabao 2-0 ili kusonga mbele katika hatua inayofuata.
Mchezo huo
ambao uliokuwa na ufundi mkubwa kwa timu zote mbili, timu ya Mali ilikuwa ya
kwanza kuandika bao kupitia kwa kiungo Ousmane Diakite.
Wakati
Ngorongoro ikicheza kwa juhudi zote kutafuta bao la kusawazisha,ndipo
mshambuliaji Dianka wa Mali alipoipatia timu yake bao la pili kunako dakika ya
40.
Ngorongoro
iliamka na kuanza kucheza kwa kasi ikitafuta bao, hata hivyo juhudi hizo
zilianza kuzaa matunda baada ya mshambuliaji Paul Peter kufunga bao la kufutia
machozi na kurudisha matumaini kwa Watanzania.
Kipindi cha
pili kilianza kwa timu hizo kushambuliana kwa zamu na kujilinda zaidi ambapo
mpaka dakika 90 zinamalizika matokeo yalibaki kwa Ngorongoro kupoteza kwa idadi
hiyo ya mabao.
No comments:
Post a Comment