WAZIRI wa Habari,
Sanaa, Utamduni na michezo, Dk Harrison Mwakyembe ameagiza kukamatwa kwa wasanii
wa muziki wa kizazi kipya Faustina Charles ‘Nandy’ na Nasib Abul
‘Diamond’ baada ya kusambaa kwa video zake chafu na kufikishwa kituo cha polisi
kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi zaidi.
Kauli hiyo
imekuja baada ya Mbunge wa jimbo la Ulanga,
Morogoro, Goodluck Mlingwa kuuliza ni hatua gani za serikali zimechukuliwa
ili kupambana na wasanii wanaweka picha za uchi na matusi katika mitandao.
Dk.Mwakyembe
amethibitisha kuwa msanii Diamond bado yuko polisi alikofikishwa tangu juzi kwa
ajili ya mahojiano baaada ya kuvujisha video akiwa na wanawake tofauti faragha.
Aidha Dk.
Mwakyembe alisema Nandy naye atahojiwa na polisi kufuatia video yake ya faragha
akiwa na msanii mwenzake Billnass kusambaa mitandaoni.
“Tulitunga sheria mwaka 2010 lakini tulikosa
sheria za kubana wasanii katika maudhui hasa katika upande wa mitandao,
tumeshatunga hizo kanuni na sasa zimeanza kufanya kazi,”
”Kuna baadhi ya vijana wamekuwa wakifanya
uhuni uhuni katika mitandao ya kijamii sana na tumeanza kuwafanyia kazi , yupo
msanii Diamond ambaye amefikishwa polisi tangu jana (juzi) kutokana na
kusambaa kwa picha zake chafu, hata hivyo pia binti Nandy pia inabidi akamatwe
ahojiwe,” alisema Dk Mwakyembe.
No comments:
Post a Comment