KOCHA Mwinyi Zahera Mkongoman mwenye uraia wa Ufaransa ametua nchini kwa
ajili ya kuifundisha Yanga huku akitamba kuishikisha adabu Simba kwenye mchezo
wa Aprili 29 unaotarajiwa kuchezwa
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Taarifa kutoka Yanga zinasema kocha huyo aliondoka jana Dar es Salaam kwenda Morogoro ambako timu hiyo imeweka kambi kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Simba.
Zahera alikuwa kwenye benchi la ufundi la timu ya taifa ya DRC, The Leopard na amewahi kufundisha soka nchini Ufaransa.

Ujio wa Zahera unadhibitisha kuwa Yanga imeachana rasmi na
Mzambia George Lwandamina aliyerejea kwao wiki mbili zilizopita kukamilisha
mipango ya kujiunga tena na klabu yake ya zamani, Zesco United baada ya
kuitumikia Yanga tangu Novemba mwaka 2016
Zahera anakuja Yanga akitoka timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambako alikuwa msaidizi wa Florent Ibenge tangu Sep 30, mwaka jana pia amewahi kuzifundisha DC Motema Pembe ya DRC tangu Machi 1, mwaka 2015 hadi Machi 10, 2016.

Pia aliwahi kuwa kocha msaidizi wa AFC Tubize ya Ubelgiji
kati ya Oktoba 7 na Oktoba 23, mwaka 2014 ambayo alijiunga nayo baada ya
kuachana na timu ya taifa ya DRC kati ya Agosti 14 na 28, mwaka 2017 chini ya kocha
Ibenge.
Zahera alizaliwa Oktoba 19, mwaka 1962 kabla ya kuanza soka mwaka 1975 akiichezea klabu ya Bankin ya Goma, Kaskazini mwa jimbo la Kivu, DRC hadi mwaka 1980.
Baadaye akaenda Kinshasa kucheza soka na kujiendeleza kielimu, akijiunga na Chuo cha Teknolojia (ISTA) huku akichezea klabu ya Sozacom hadi alipokutana na wakala wa wachezaji, Mbelgiji Karl Broken aliyemchukua na kumpeleka Ulaya kucheza soka ya kulipwa.
Zahera alicheza kwa misimu miwili Antwerp FC ya Ubelgiji kabla ya kumaliza mkataba wake na kwenda Ufaransa alikochezea timu za Daraja la Pili, Amiens, Beauvais na Abbeville hadi akastaafu soka.
Baada ya hapo akaanza kupata mafunzo ya ukocha ambako alitunukiwa advance na leseni C, B na A za Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA)

Amewahi kuifundisha klabu ya SC Feignies ya Ufaransa kuanzia
mwaka mwaka 2000 hadi 2010 kwa mafanikio makubwa kabla ya kwenda Ubelgiji kuifundisha
Tubize na baadaye kurejea DRC na sasa amekuja kujaribu maisha mapya Tanzania.
Kwa sasa Yanga ipo kambini Morogoro kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa siku ya Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Yanga inazidiwa kwa pointi 11 na Simba lakini ina viporo viwili na ili kutetea ubingwa inalazimika kushinda mechi zote zilizobaki za ligi kuu na Simba ipoteze mechi mbili jambo ambalo ni ngumu kutokana na uwezo wake kwani haijafungwa.

No comments:
Post a Comment