TIMU ya
Taifa ya Vijana U-17, Serengeti Boys, kesho inatarajia kutupa karata yake muhimu
kwenye mchezo wa nusu fainali wa mashindano ya CECAFA dhidi ya Kenya.
Mchezo huo
utachezwa saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Muyinga nchini Burundi.
Serengeti
Boys imefuzu nusu fainali baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Uganda
kwenye mchezo wa kwanza na kuifunga Sudan kwa mabao 6-0 kwenye mchezo wa mwisho
wa makundi
Akizungumza
kocha wa Serengeti boys, Oscar Mirambo alisema mchezo dhidi ya Kenya utakuwa wa
ushindani lakini kutokana na maandalizi waliyofanya na ari waliyonayo wachezaji
watashinda.
“Tumefanya
maandalizi ya kutosha, tunaamini tutafuzu fainali na ni nia yetu kushinda na
kurudi na ubingwa huu,” alisema Oscar.
Wakati huo
huo timu ya Taifa ya Vijana waliochini ya umri wa miaka
20,
Ngorongoro Heroes imerejea nchini leo ikitokea nchini DR Congo kwenye mchezo
wa marudiano wa kufuzu fainali za Africa za Vijana U-20 dhidi ya DR Congo
ilishinda kwa penalti 6-5 baada ya suluhu katika dakika 90 za mchezo.
Baada ya
kurudi wachezaji wote wamepewa mapumziko ya siku tatu na wakirejea wataendelea
na program ya kocha mkuu Ammy Ninje kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa raundi
ya pili dhidi ya Mali utakaochezwa mwezi ujao mchezo ambapo wataanzia nyumbani.
No comments:
Post a Comment