MABINGWA
watetezi wa kombe la Muungano kwa upande wa wanawake, timu ya Tanzania Prisons
imeanza vema kutetea ubingwa wao baada ya kuifunga JKT kwa seti 3-0 katika
mchezo uliochezwa jana katika viwanja vya Ziwani, Zanzibar.
Akizungumza
kwa njia ya simu toka Zanzibar, nahodha wa timu hiyo Hellen Richard alisema wanashukuru
kwa kupata ushindi huo kwani JKT ni moja ya timu ambayo walikuwa wanaiogopa.
“Tunashukuru
kupata ushindi katika mchezo wa kwanza kwani ni mwanzo mzuri wa kutetea ubingwa
ukizingatia JKT ni timu nzuri,” alisema Hellen
Kwa upande
wa timu za wanaume, Faru imeshinda michezo yake miwili ambapo iliifunga Nyuki
ya Zanzibar kwa seti 3-1 na kuifunga Mafunzo kwa seti 3-2.
Pentagone
imecheza michezo miwili ikashinda mchezo mmoja na kupoteza mmoja ambapo
iliifunga Nyuki kwa seti 3-1 na kufungwa na Polisi kwa seti 3-2 pia Polisi
ikaifunga JKT kwa seti 3-0, ikaifunga Mafunzo seti 3-2 na kuifunga Nyuki seti
3-0.
Kwa upande
wa wanawake JKT baada ya kufungwa na Tanzania Prisons iliifunga Polisi ya
Zanzibar kwa seti 3-0.
Timu
zinazoshiriki kwa upande wa wanaume ni Polisi, Nyuki na Mafunzo za Zanzibar,
JKT, Faru na Pentagone za Tanzania Bara na kwa upande wa wanawake ni Polisi
Zanzibar, JKT na Tanzania Prisons za Bara.
Kwa upande
wa wanaume bingwa mtetezi Jeshi Stars hajashiriki msimu huu hivyo kombe haki
sasa halina mwenyewe.
No comments:
Post a Comment