TIMU ya taifa ya
vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya Tanzania, Ngorongoro Heroes, imetoa
zawadi kwa Watanzania baada ya kuifunga Morocco 1-0 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini
Dar es Salaam.
Bao hilo pekee
lililoitoa kifua mbele Ngorongoro Heroes, lilifungwa na Muksin Makame katika
dakika ya 73 kwa penalti baada ya mlinzi wa Morocco Limourt Youssef kuunawa
mpira katika eneo la hatari.
Katika mchezo huo wa
kimataifa wa kirafiki, timu hizo zilicheza kwa kushambuliana kwa zamu, huku
zikitoa burudani safi kwa watazamaji walioingia bure uwanjani.
Baada ya mchezo huo, Ngorongoro
Heroes Jumatano watacheza dhidi ya Msumbiji katika mchezo mwingine wa kirafiki
kujiandaa na mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
Pamoja na kuwa ni
mchezo wa kirafiki, lakini ushindi huo ni muhimu kwa Ngorongoro kwani timu za
Tanzania kuanzia zile za klabu na taifa zimeshindwa kabisa kuzifunga timu za
Morocco.
Kikosi cha Ngonrongoro: Aboutnalib Msheli, Kibwana Shomary, Nickson Kibabage,
Ally Msengi, Dickson Job, Ally Ngazi, Hassadi Juma, Kelvin Naftal, Maziku Aman,
Abdul Seleiman na Said Bakari.
No comments:
Post a Comment