YANGA leo imeifunga Saint Louis ya Shelisheli bao 1-0 lakini imejiweka pabaya kwani sasa
italazimika kushinda ama kulinda bao lake ili wenyeji wasipate bao katika mechi
ya marudiano Shelisheli wiki ijayo.
Juma Mahadhi
ndiye aliyeifungia Yanga bao hilo pekee katika mechi hiyo ya awali ya michuano
ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyochezwa uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mahadhi
alifunga bao hilo katika dakika ya 67 ikiwa ni dakika moja tangu alipoingia
uwanjani kuchukua nafasi ya Ibrahim Ajibu.
Mahadhi
alifunga bao hilo akiunganisha kona iliyochongwa na Geofrey Mwashiuya.
Mapema
dakika ya 24 Obrey Chirwa aliikosesha Yanga bao baada ya mkwaju wa penalti
aliopiga kwenda pembeni.
Penalti hiyo
ilitolewa na mwamuzi baada ya Hassan Kessy kuangushwa eneo la hatari.
Kwa ujumla
katika mechi ya jana, wapinzani wa Yanga waliingia kuzuia hali iliyowapa ugumu
washambuliaji wa Yanga kuipenya ngome yao, hasa katika kipindi cha kwanza.
Katika
kipindi hicho cha kwanza, Yanga ilikosa mabao katika dakika ya 16, Pius Buswita
alikosa baada ya kupiga vibaya mpira wa kona, Emmanuel Martin naye akiwa kwenye
nafasi nzuri ya kufunga katika dakika ya 19, alipaisha mpira.
Ajibu naye
alishindwa kufunga dakika ya 41 na dakika ya 43, Papy Tshishimbi naye
alishindwa kufunga akiwa kwenye nafasi nzuri ya kufanya hivyo.
Kutoka
kwenye uwanja wa Amaan Zanzibar, mwandishi Wetu Mwajuma Juma anaripoti kuwa
wenyeji JKU wametoka suluhu na Zesco ya Zambia katika michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment