BARAZA la Michezo nchini (BMT) limesema shughuli
za Michezo nchini zinafanyika kwa mujibu wa sheria ya Baraza la Michezo la
Taifa namba 12 ya mwaka 1967 na marekebisho yake ya sheria namba 6 ya mwaka
1971.
Hayo yamesemwa jana na Ofisa habari wa BMT, Frank Mgunga, na kuongeza kila
chama, shirikisho, klabu au asasi na taasisi zina miongozo mbalimbali
inayosaidia kuendesha michezo katika maeneo yao.
“Katika kutekeleza shughuli za michezo kama mashindano,
yamekuwa yakiibuka malalamiko au migogoro ambayo kwa namna moja au nyingine
inahitaji utatuzi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu stahiki hasa kwa
vyama vilivyosajiliwa,” alisema Mgunga
Mgunga alisema zipo taratibu za kufuata katika
kuwasilisha malalamiko Malalamiko au rufaa na Mchezaji, Kiongozi, Chama, Klabu,
Mwalimu, Mwamuzi, Daktari wa Timu au
mdau mwingine wa michezo anao uhuru na haki ya kuwasilisha malalamiko yake kwa
kufuata utaratibu kwa ngazi ya juu endapo hakuridhika na uamuzi uliotolewa na
Uongozi wa Ngazi husika.
“Malalamiko yatapelekwa kwa Chama cha Mchezo husika na
kwa mujibu wa Kanuni za mchezo husika na nakala yake itapelekwa katika Kamati
ya Michezo ya Wilaya katika muda usiozidi siku tatu baada ya uamuzi kutolewa,”
alisema Mgunga
Pia alisema kama mlalamikaji hataridhika atakata rufaa
kwa Kamati ya Nidhamu, Rufaa na Usuluhishi ngazi ya Wilaya katika muda usiozidi
siku saba na kama hataridhika na uamuzi atakata rufaa kwa Kamati ya Michezo ya
Mkoa katika muda usiozidi siku saba
Aidha endapo hataridhika na uamuzi wa Baraza atakuwa na
haki ya kukata rufaa kwa Waziri katika muda wa siku saba na maamuzi ya Waziri
yatakuwa ya mwisho.
Katika Ngazi Mkoa na Taifa utaratibu utafuata mtiririko wa ngazi ya
wilaya kupata haki hivyo Vyama
vyote, mashirikisho na klabu na wadau wa michezo mnasisitizwa kufuata utaratibu
huu ambao ni muhimu ili kutoruka ngazi katika kuimarisha Utawala Bora.
No comments:
Post a Comment