SIMBA kesho inashuka kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kucheza mechi ya kimataifa kwa
mara ya kwanza baada ya miaka takriban mitano.
Vinara hao
wa Ligi Kuu Bara, wataikabili Gendarmerie ya Djibouti katika mechi ya hatua ya
awali ya michuano ya kombe la Shirikisho Afrika.
Simba
inashuka kwenye mchezo huo huku ikiwa na mwendo mzuri kwenye mechi za Ligi Kuu
Bara baada ya kucheza mechi 17 ikiwa kileleni mwa msimamo kwa kufikisha pointi
41 bila kufungwa mechi hata moja.
Mchezo huo
ni muhimu kwa Simba kuibuka na ushindi ili kujitengenezea mazingira mazuri ya
kusonga mbele hatua inayofuata kwani itatakiwa kucheza mchezo wa marudiano wiki
ijayo ugenini. Djibouti.
Akizungumza
na gazeti hili, Kocha wa Simba, Pierre Lechantre alisema kuwa mchezo huo ni
muhimu kwa upande wao na anachokihitaji ni ushindi.
Alisema kuwa
tayari alishazinasa CD za mechi zilizopita za wapinzani hao na kuzifanyia kazi
hasa mbinu wanazozitumia, hivyo haitakuwa ngumu kwao kukabiliana nao.
Aliongeza
kuwa atafanya kila awezalo kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo kwani anajua
wanachohitaji Simba kwa sasa ni ushindi katika kila mechi, hivyo na yeye
anataka kuhakikisha anawapa kile wanachokihitaji.
“Nilishapata
mbinu zao muda mrefu sana na nilisha zifanyia kazi kuona nakabiliana nao kwa
staili ipi, nitahakikisha hawatoki salama kama mechi ni bora nimalize hapa hapa
Tanzania hata nikienda kwao tusiwe na wasiwasi kuwa labda watatutoa.
“Nimekuja
Simba kwa kazi moja tu ya kuipa mafanikio, hivyo mtihani mwingine ni huu kwenye
mechi yangu ya kwanza ya kimataifa na hivyo nahitaji kujenga imani kwa
mashabiki wa Simba,” alisema Lechantre.
No comments:
Post a Comment