WAZIRI wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ametua
kamati ya kusimamia ngumi za kulipwa nchini Tanzania.
Akizungumza
jana, Katibu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Mohamed Kiganja alisema kamati
hiyo ina wajumbe 12 na itakuwa ikisaidia Baraza la Michezo la Taifa kuratibu
shughuli za kila siku za ngumi za kulipwa nchini Tanzania
“Januari 3,
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe aliteua
wajumbe kumi na mbili kuunda kamati ambayo ingetengeneza Rasimu ya katiba ya
chombo cha kusimamia ngumi za kulipwa nchini Tanzania na ilikabidhi rasimu
Februari 3,” alisema Kiganja.
“Baada
kuipokea Rasimu hiyo aliipongeza na kuishukuru kamati hiyo kwa kazi nzuri iliyofanya kwa umahiri na
kujitoa kwa muda wao na kuahidi kuwa atateua kamati nyingine ambayo ndio hii
ninaitangaza leo,” aliongeza Kiganja
Kamati hiyo Mwenyekiti
Emmanuel Saleh, Makamu Mwenyekiti ni Joe Anea na Katibu ni Yahya Poli
Wajumbe ni
Habib Kinyogoli, Rashid Matumla, Anthony Ruta, Shomari Kimbau, Dk.Killaga
Killaga, Karama Nyilawila, Fike Wilson, Jaffar Ndame na Ali Bakari
Kigamnja
alisema kamati hiyo itapokea maoni kwa maandishi kutoka kwa wadau wa ngumi
katika kipindi cha mwezi mmoja kupitia tovuti ya Baraza la Michezo la Taifa
ambayo ni www.nationalsportscouncil.go.tz
na tovuti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo www.habari.go.tz
Pia
itaratibu mkutano wa kujadili rasimu katika kipindi cha miezi miwili ili kuwapa
wadau waliokosa nafasi kwa njia ya maandishi kutoa maoni yao na kuandaa mkutano
mkuu wa uchaguzi.
No comments:
Post a Comment