Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, November 4, 2017

WACHEZAJI 16 NA BENCHI LA UFUNDI WA POLISI DAR ES SALAAM WASIMAMISHWA

KAMATI ya Bodi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (kamati ya saa 72) imeanza kazi kwa kuwasimisha wachezaji 16 na benchi la ufundi wa Polisi Dar es Salaam ambayo inacheza ligi daraja la kwanza pamoja na kipa wa Mbeya City Owen Chaima.
Akizungumza Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Lucas alisema kipa Owen amesimamishwa kwa kosa la kumpiga kofi mchezaji wa Azam FC wakati wa mchezo dhidi yao uliochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex Oktoba 27.
“Uamuzi wa kumsimamisha Owen umefanywa na kamati kwa kuzingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu na shauri lake limeletwa kwenye Kamati ya Nidhamu TFF na litasikilizwa Novemba 7, saa 10.00 jioni,” alisema Lucas.
Pia Lucas alisema wachezaji 16 wa Polisi Dar ambao ni Mpokigwa Mwafubela , Emmanuel Mwita, Mateso Baraka, Magige Belence, Ally Mustafa, Henerico Sylvanus, Paul Makula, Paschal Theodory, Evance Wilfred, Kulwa Manzi, Athumani Mrisho, Erick Mongi, Damson Mabala, Shabani Juma na Innocent Barisidya wamesimamishwa kwa kosa la kumpiga mwamuzi.
“Wachezaji hao pamoja na viongozi wa timu hiyo kocha mkuu William John, kocha msaidizi Thabit Kapula, kocha wa makipa Eliud Mwalugelo, mtunza vifaa Iman Naftari wamesimamishwa kwa mujibu wa kanuni ya 9(5) ya ligi daraja la kwanza na kiongozi wao Mathias Mrimi kwa kuhamasisha vurugu dhidi ya mwamuzi  hadi Kamati ya Nidhamu ya TFF itakaposikiliza shauri,” alisema Lucas.
Pia Kocha Msaidizi wa JKT Mlale, Rashid Mpenda pamoja na Meneja wa timu hiyo Issa Ngwasho wamesimamishwa kwa kosa la kumvamia mlemavu wakimtuhumu kwa ushirikina, Mtunza Vifaa wa Mawenzi Market, Jumanne Mohamed kwa kosa la kutaka kumdhuru Mwamuzi, wachezaji wa Mawenzi Market, Ayubu Isaya Sijila, Abdallah Kulandana na Juma Sekubo wamesimamishwa kwa kosa la kumpiga mwamuzi
Wengine waliosimamishwa ni wachezaji Shaibu Ally na Frank Kijoti wa JKT Oljoro pamoja na Kocha wao Emmanuel Masawe wamesimamishwa kwa kosa la kumfukuza na kutaka kumpiga mwamuzi na mashauri dhidi yao yatasikilizwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF Novemba 7, saa 10.00 jioni kwenye ofisi za TFF, Karume, Ilala Dar es Salaam.
Katika ligi daraja la pili kocha wa AFC, Gerald Totoo,  Kipa wa AFC, Aladini Hashimu, mchezaji Christopher Castor wa African Sports, wachezaji wa JKT Msange, Hosea John , Rashid Ally, Hamis Athuman, Casmir Focus pamoja na mtunza vifaa wa timu hiyo Erick Paul, mchezaji Katregea Kalegea wa Mashujaa FC  wamesimamishwa hadi kamati ya nidhamu itakaposikiliza mashauri yao.
Wengine ni kocha msaidizi wa Area C, Omarooh Omari aliyempiga kiwiko mchezaji Rajabu Adam wa Nyanza FC alipokuwa akikimbilia mpira uliopita karibu na kocha huyo.

No comments:

Post a Comment