SHIRIKISHO
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limesema limezilipa timu zote sita
zinazotarajiwa kushuka dimbani leo katika michezo ya awali ya kufungua dimba
michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam ‘Azam Sports Federation Cup’ (ASFC).
Akizungumza,
Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Lucas alisema timu
hizo ni Buseresere ya Geita itakayocheza na Isako ya Songwe, Usamala ya Simiyu
ambayo itacheza na Sahale All Stars ya Tanga na Kisarawe United ya Pwani na
Silabu ya Mtwara ambao umeahirishwa kwa
sababu ya majeruhi ya wachezaji baada ya kupata ajali.
“Timu za
Buseresere, Isako, Usamala, Sahale All Stars, Kisarawe na Silabu zote zimelipwa
pesa zao na kesho (leo) zinatarajiwa kushuka dimbani kucheza isipokuwa Kisarawe
na Silabu umeahirishwa kwasababu Silabu walipata ajali wakiwa safarini kwenda
Pwani.
Baada ya
mechi hizo, itakuja raundi ya kwanza ya ASFC ambayo itachezwa kati ya Novemba
7, 8 au 9 ambako TFF imepanga leo kutuma fedha zote za maandalizi ya timu
husika ili kusiwe na kisingizio chochote cha kujiandaa.
Lucas
alisema Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Kidao Wilfred ameagiza Idara ya Fedha na
Utawala ya TFF kulipa fedha hizo haraka kwa kufuata taratibu za malipo kupitia
benki, badala ya akaunti ya mwakilishi ye yote au kiongozi.
Pia Kidao
ameagiza timu ambayo haijafungua akaunti watakuta fedha zao kwa Chama cha Mpira
wa Miguu Mkoa (FA), lakini TFF ingependa kusisitiza kwa wadau hao kufufua
akaunti au kufungua akaunti haraka.
Katika
raundi ya kwanza Mashujaa ya Kigoma itacheza na Mshindi kati ya Buseresere ya
Geita na Isako ya Songwe, wakati mechi
nyingine Msange ya Tabora itacheza na Milambo pia ya Tabora na Bulyanhulu ya
Shinyanga itacheza na Area C ya Dodoma.
Mji Mkuu FC
ya Dodoma itacheza na Nyundo ya Kigoma wakati Baruti FC ya Mara itacheza na
Ambassodor ya Kahama, Shinyanga huku Eleven Stars ya Kagera ikipangwa kucheza
na Ndovu ya Mwanza.
Changanyikeni
ya Dar es Salaam itacheza na Reha FC pia ya Dar es Salaam wakati mshindi kati
ya Kisarawe United na Silabu ya Mtwara atacheza na Kariakoo ya Lindi huku
Cosmopolitan ikicheza na Ajabalo wakati Makumba FC itacheza na Green Warriors
ya Kinondoni, Namungo FC ya Lindi itachuana na Villa Squad ya Dar es Salaam
huku Dar City ikicheza na Majimaji Rangers ua Nachingwea.
Michezo mingine
ya hatua ya kwanza itakutanisha timu za Shupavu FC ya Morogoro na Sabasaba pia
ya mjini humo, Motochini FC ya Katavi dhidi ya Ihefu FC ya Mbeya, The Mighty
Elephant ya itacheza na Makanyagio ya Rukwa.
Burkina FC
ya Morogoro itacheza na Mbinga United ya Ruvuma, Makambako Heroes ya
Njombe itacheza na Mkamba Rangers ya Morogoro, Real Moja Moja itapambana
na African Wonderers – zote za Iringa. Boma FC ya Mbeya itacheza na African
Sports ya Tanga.
Mechi
nyingine za hatua hiyo itakuwa ni kati ya Pepsi ya Arusha ambayo itacheza na
Kilimanjaro Heroes ya Kilimanjaro, Stand Misuna ya Singida itacheza na Madini
FC ya Arusha, AFC ya Arusha itacheza na Nyanza ya Manyara, New Generation
itacheza na Mshindi kati ya Usamala FC na Sahale ya Tanga. Bodaboda FC itacheza
na Kitayose ya Kilimanjaro.
Michuano
hiyo ambayo Bingwa Mtetezi ni Simba ya Dar es Salaam, inashirikisha timu 91
msimu huu kwa mchanganuo wa timu 16 za Ligi Kuu Tanzania Bara, 24 za Ligi
Daraja la Kwanza, 24 za Ligi Daraja la Pili na 27 za Ligi ya Mabingwa wa Mkoa
No comments:
Post a Comment