KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za
Michezo Tanzania (TASWA), iliyokutana Dar es Salaam hivi karibuni, imeteua
wanahabari tisa kuunda Kamati ya Marekebisho ya Katiba ya chama.
Wengi wa
walioteuliwa ni wanachama wa TASWA na wengine ni viongozi wa zamani wa chama na
pia baadhi ni wanahabari wa michezo.
Mwenyekiti
wa kamati hiyo atakuwa ni Mwenyekiti wa zamani wa TASWA, Boniface Wambura
ambaye licha ya kuwa mwanahabari pia ana taaluma ya sheria na kwa sasa ni Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB) na Katibu wa Kamati atakuwa Wakili
Emmanuel Muga.
Wajumbe ni
Katibu Mkuu wa zamani wa TASWA, Abdul Mohammed wa gazeti la Mwananchi, Mhazini
Msaidizi wa zamani wa TASWA ambaye kwa sasa ni Mhariri wa michezo wa gazeti la
Daily News, Nasongelya Kilyinga.
Wajumbe wengine ni Florian Kaijage kutoka Azam Media, Mahmoud
Zubeyri kutoka Bin Zubeyri Blogs, Tunu Hassan wa EFM Redio, Benny
Kisaka wa Jambo Concept na Majuto Omary wa gazeti la Citizen.
Hatua ya
kuunda kamati hiyo inatokana na maelekezo kutoka Baraza la Michezo la Taifa
(BMT), ambalo limetaka chama kifanye marekebisho ya katiba kwanza
ili iwe rahisi kwa mambo mengine yafanyike katika utaratibu mzuri ikiwa ni
pamoja na Uchaguzi Mkuu wa chama.
Kutokana na
hali hiyo, Kamati ya Utendaji imekabidhi jukumu hilo kwa Kamati Maalum ambayo
itapanga utaratibu wake wa namna ya kufanyia marekebisho katiba hiyo, ikimaliza
itawasilisha rasimu ya Katiba kwenye Mkutano Mkuu wa chama kwa hatua
nyingine.
Ni imani ya
Kamati ya Utendaji kwamba Kamati ya Katiba inaweza kukamilisha rasimu hiyo
katika muda usiozidi siku 90, ikiwa chini ya hapo itakuwa vizuri zaidi.
Tunaomba
wadau wote tuipe ushirikiano wa namna mbalimbali kwa kadri itakavyowezekana ili
tupige hatua katika kuimarisha chama chetu.
Nawasilisha,
Amir Mhando
Katibu Mkuu
TASWA
24/11/2017
No comments:
Post a Comment