SHIRIKISHO
la Soka barani Afrika (CAF) limesogeza mchezo wa kufuzu mataifa ya Afrika
(AFCON) kati ya Tanzania na Uganda kupisha timu za Taifa zilizofuzu fainali ya Kombe
la Dunia zitakazofanyika Urusi 2018 kujiandaa.
Mchezo huo
awali ulikuwa huchezwe Machi 2018 lakini umesogezwa hadi Septemba 2018.
Taarifa ya
CAF inasema mchezo huo ulikuwa huchezwe Machi 18 hadi 26 lakini sasa utachezwa
Septemba 3 hadi 11.
Tanzania ipo
Kundi L pamoja na timu za Cape Verde,
Uganda na Lesetho.
Kila timu
imecheza mchezo mmoja huku Tanzania ikiwa imecheza nyumbani na Lesotho na
kutoka sare ya bao 1-1.
No comments:
Post a Comment