SIMBA imefanikiwa kurejea kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya
kuifunga Mbeya City bao 1-0 katika uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya
Iliichukua Simba dakika saba kupata bao lililofungwa na Shiza
Kichuya baada ya kupokea mpira uliopigwa
na Jonas Mkude ambaye alipokea pasi kutoka kwa Haruna Niyonzima aliyepiga mpira
wa adhabu ndogo.
Katika kipindi cha kwanza Simba ilitawala mchezo na kufanikiwa
kuliandama lango la Mbeya City huku dakika ya 43 Erasto Nyoni akikosa bao la wazi
na kumaliza dakika 45 wakiwa na bao hiyo moja.
Kipindi cha pili Mbeya City walianza mchezo kwa kasi na kuliandama lango
la Simba ambao walicheza mchezo wa kujihami muda mwingi lakini umakini wa kipa
Aishi Manura walijikuta mipira ikiishia mikoni mwake.
Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 19 baada ya kucheza mechi
tisa na kupanda kileleni ikiizidi kwa wastani wa mabao Azam yenye pointi 19 pia
na Yanga wakishika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 18 sawa na Mtibwa Sugar
baada ya juzi kutoka sare.
Simba itasalia Mbeya hadi Novemba 18 itakapocheza na Tanzania Prisons
katika mchezo wa ligi kuu na Jumamosi inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na
Kyela kombaini kwenye Uwanja wa Mwakangale kabla ya kuivaa Prisons.
Kichuya
amefikisha mabao matano (5) kwenye ligi sawa na Ibrahim Ajib wa Yanga huku
akiwa anaziwa na Mohamed Rashid wa Tanzania Prisons mwenye mabao sita na
Emanuel Okwi wa Simba anaeongoza akiwa na mabao nane.
Simba
imeshinda mechi ya tatu kati ya tano ilizokutana na Mbeya City kwenye Uwanja wa
Sokoine, Mbeya, kabla ya mchezo wa leo, Simba ilikuwa imeshinda mechi mbili
kati nne, mchezo mmoja walitoka sare na mwingine walipoteza.
Mbeya City
imepoteza mchezo wa pili kati ya mechi tano walizocheza kwenye uwanja wa
Sokoine. Mchezo mwingine waliopoteza kwenye uwanja wa Sokoine ilikuwa dhidi ya
Ndanda.
Kikosi cha Simba kilikuwa Aishi Manula, Erasto Nyoni, Mohamed Hussein
‘Tshabalala’, James Kotei, Juuko Murshid, Jonas Mkude, Shiza Kichuya/Mohammed
‘Mo’ Ibrahim dk 88, Muzamil Yassin/Laudit Mavugo dk 78, John Bocco, Emmanuel
Okwi na Haruna Niyonzima /Said Ndemla dk55.
Kikosi cha Mbeya City kilikuwa ni Fikirini Bakari, Erick Kyaruzi, Hassan
Mwasapili, Ally Lundenga, Sankan Mkandawile, Babu Ally, Mrisho Ngassa, Mohammed
Samatta, Mohammed Mkopi/Victor Hangaya dk 82, Omary Ramadhani/Iddi Nado dk 64
na Eliud Ambokile.
Katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Samora Iringa wenyeji Lipuli FC wametoka sare ya bao 1-1 na Mwadui FC
Katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Samora Iringa wenyeji Lipuli FC wametoka sare ya bao 1-1 na Mwadui FC
Wenyeji Lipuli FC walipata bao
dakika ya 48 lililofungwa na Asante Kwasi kwa penalti lakini Mwadui FC
wakasawazisha dakika ya 70 bao lililofungwa na Abdallah Seseme .
No comments:
Post a Comment