WAAMUZI
watatu wa Kimataifa wa Tanzania wameteuliwa kuchezesha mashindano ya Chalenji
yanayotarajiwa kufanyika Nairobi Kenya kuanzia Desemba 3-17.
Akizungumza
na Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA)
ambao ndio waandaji wa mashindano hayo aliwataja waamuzi hao kuwa ni Elly
Sasii, Nassor Mfaume na mwamuzi msaidizi Soud Lila.
“Waamuzi
watakaochezesha Chalenji wapo 16, nane waamuzi wa kati na nane waamuzi
wasaidizi na watatu wanatoka Tanzania. Septemba 29 wanatakiwa kuwa wamefika
Nairobi kwani Septemba 30 na Desemba Mosi watafanya mtihani wa utimamu,”
alisema Musonye.
Waamuzi
wengine ni George Gotagota na Abdoul Karim (Burundi), Peter Waweru na Anthony
Ogwayo (Kenya), Alex Muhabi (Uganda) na Malong Akech (Sudan Kusini)
Waamuzi
wasaidizi ni Herve Kakunze (Burundi), Tigle Belachew (Ethiopia), Ndagijimana
Theogene (Rwanda), Tony Kidiya na Joshua Achila (Kenya), Dick Okello na Ronald
Katenya (Uganda)
Mashindano
ya Chalenji yanatashirikisha timu kumi ambazo ni Tanzania, Zanzibar, Uganda,
Somalia, Sudan, Ethiopia, Sudan Kusini, Burundi, Rwanda na wenyeji Kenya.
No comments:
Post a Comment