KUTOKANA na
ushindani wa namba uliopo kwenye klabu ya Singida United kocha Hans Pluijm
amekubali kumtoa kwa mkopo mshambuliaji wake Pastory Athanas, kwenda Stand
United
Akizungumza Kocha
Hans Pluijm alisema amekubali maombi ya Stand United, kwa sababu mchezaji huyo
amekuwa hapati nafasi tangu walipomsajili mwanzoni mwa msimu huu akitokea
Simba.
“Nimekubali
Athanas aondoke ili kulinda kipaji kwasababu mchezaji asipopata nafasi ya
kucheza kiwango kitashuka,” alisema Pluijm.
Athanas
ametolewa kwa mkopo na uongozi wa Singida United unasema umekubaliana na Simba
na umefanya kwa faida ya pande zote tatu, yaani Simba, Singida na mchezaji
mwenyewe.
Katibu Mkuu
wa Stand United, Kenedy Mwangi alikiri kufanya usajili wa wachezaji wanne,
watatu wa kimataifa na mmoja ni Athanas lakini akakataa kuwataja majina kwa
kuhofia kutibuliwa kwa vile kuna taratibu hazijakamilika.
“Tumejipanga
kusajili wachezaji wanne, wawili Warundi, Mganda mmoja na Mtanzania mmoja ambao
wanacheza namba tano, nane na tisa, baadhi ya taratibu zimekamilika na nyingine
bado hivyo zikikamilika tutaweka majina yao hadharani,” alisema Mwangi
No comments:
Post a Comment