MSANII
wa Bongo Muvi, Irene Uwoya amesema ni kipindi kigumu kwake kuondokewa na
aliyekuwa mume wake, Hammad Ndikumana Katauti.
Habari
za kifo cha Ndikumana zilianza kusambaa jana asubuhi kwenye mitandao mbalimbali
ya kijamii ikiwemo Instagram.
Gazeti
hili lilizungumza na Uwoya ambaye anaomboleza msiba wa mzazi mwenzake nyumbani
kwake Sinza Mori, Dar es Salaam na kusema: “ Imeniuma, Hammad ni mzazi
mwenzangu, baba wa mtoto wangu, pamoja na tofauti zetu, bado ni baba wa
mwanangu mpendwa, ”alisema Uwoya huku akiangua kilio na watu mbali mbali
wakiwemo wasanii wa filamu walikusanyika nyumbani kwa msanii huyo.
Alisema
anangalia utaratibu ili yeye na mtoto wake waweze aweze kwenda kuhani msiba wa
mumewe huyo wa zamani ambaye ni mzaliwa wa Burundi, lakini alicukua uraia wa
Rwanda.
Ndikumana
alifunga ndoa ya kikristo na Uwoya mwaka 2009 na kufanikiwa
kupata mtoto mmoja wa kiume waliyempa jina la Krish, lakini ndoa yao
haikudumu kwa muda mrefu wakatengana, ambapo hivi karibuni kulitoka taarifa
kwa Irene kufunga ndoa na Abdulaziz Abubakari ‘Dogo Janja’.
Kwa
mujibu wa Ofisa Habari wa Rayon Sports ya Rwanda, Gakwaya Olivier alisema Ndikumana
ambaye alikuwa Kocha Msaidizi wa timu hiyo alifariki ugonjwa wa moyo.
Akizungumzia
msiba huo, kiungo wa Simba ya Dar es Salaam, ambaye ni raia wa Rwanda, alisema:
“Pumzika kwa amani kaka Ndikumana, tumekupenda ila Mungu amekupenda zaidi,
hakika umetuachia majonzi makuu.”
Naye
mshambuliaji wa Yanga ya Dar es Salaam, Amiss Tambwe ambaye ni raia wa Burundi,
alisema: “Nasikitika kwa kifo cha Ndikumana, yani simani kabisa kama amekufa,
hakika kifo hakina huruma. Amekufa bado mdogo.”
Jana
mitandao ya kijamii suala al kifo cha Ndikumana lilikuwa gumzo kwa wengi
kuonesha mshtuko wa nini kimemkumba nyota huyo wa soka hadi mauti hayo
kumkumba.
Watumiaji
wa mitandao ya kijamii walikuwa wakituma ujumbe wa kumtakia apumzike kwa amani
Ndikuma na kusema wanaadamu wote njia yao ni moja.
Ndikumana
ambaye alikuwa na umri wa miaka 39 amechezea timu mbalimbali ikiwa ni pamoja na
nchini Ubelgiji na Cyprus, ambapo mwaka 2015 alisajiliwa na Stand United ya
Shinyanga inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, ingawa alikaa muda mfupi.
No comments:
Post a Comment