MCHEZAJI
Kiraka wa Simba Erasto Nyoni ameibuka mchezaji bora wa klabu hiyo kwa mwezi
Oktoba baada ya kuonesha kiwango cha juu katika mechi nne na kuzawadiwa sh
500,000.
Erasto
ambaye anamudu kucheza nafasi nyingi uwanjani amekuwa chachu ya matokeo mazuri
kwa Simba tangu asajiliwe akitokea Azam FC msimu huu.
Katika
taarifa iliyotolewa na SimbaApp inasema katika mwezi Oktoba Simba ilicheza
mechi nne na Erasto alicheza vizuri na kuisadiwa timu kupata matokeo mazuri.
“Katika
mechi dhidi ya Njombe alichangia upatikanaji wa jumla ya mabao matatu katika
mechi hizo nne tangu ligi ianze akiwa ametoa pasi sita za mabao na yeye
akifunga moja,” ilisema taarifa hiyo.
Mechi ambazo
Erasto alisaidia timu yake ni dhidi ya Stand United, Mtibwa Sugar, Njombe Mji
na Yanga ambapo walishinda mechi mbili na kutoka sare mbili.
Kuanzia ligi
inaze msimu huu tuzo ya mchezaji bora Agosti ilikwenda kwa mshambuliaji Emanuel
Okwi na Septemba ilichukuliwa na kiungo mshambuliaji Mzamiru Yassin.
Simba
imeondoka leo kwa ndege kwenda Mbeya kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania
Bbara dhidi ya Mbeya City unaotarajiwa kuchezwa Jumapili katika Uwanja wa
Sokoine.
No comments:
Post a Comment