TIMU ya soka ya
Taifa, ‘Taifa Stars’ inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi
ya Benin Novemba 11 mwaka huu, mjini Port Novo.
Akizungumza na
waandishi wa habari jana Kocha Mkuu wa Stars, Salum Mayanga alisema ameita
wachezaji 21 ambao wataingia kambini
Novemba 5 kwa maandalizi ya mechi hiyo.
"Nimeita kambini
wachezaji 21 lakini pia nimeita wachezaji chipukizi watatu kwa ajili ya kupata
uzoefu," alisema Mayanga. Wachezaji
chipukizi walioitwa ni Yohana Nkomola, Abdul Mohamed na Dickson Job. Taifa stars itaanza mazoezi Novemba 6 na
wataondoka Novemba 9 kwenda Benin. Kikosi kamili kilichoitwa ni Makipa: Aishi
Manula (Simba SC), Peter Manyika (Singida United) na Ramadhani Kabwili, mabeki
ni Boniphace Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Gardiel
Michael (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Nurdin Chona (Prisons), Erasto Nyoni
(Simba) na Dickson Job (Mtibwa Sugar).
Viungo ni Himid Mao
(Azam FC), Hamisi Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Muzamil Yassin (Simba), Raphael
Daudi (Yanga), Simon Msuva (El Jadida, Morocco), Shiza Kichuya (Simba), Ibrahim
Ajib (Yanga), Mohammed Issa (Mtibwa), Farid Mussa (Tenerife/Hispania) na Abdul
Mohammed (Tusker/Kenya) na washambuliaji Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji),
Mbaraka Yussuf (Azam FC), Elias Maguri (Huru) na Yohanna Nkomola (Huru).
No comments:
Post a Comment