SHIRIKISHO la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF ) limeandaa ligi ya mpira wa miguu wa ufukweni kwa timu
za taasisi za Elimu ya juu mkoa wa Dar es Salaam na Pwani inayotarajiwa kuanza
Novemba 9 katika Uwanja wa Karume Dar es Salaam.
Akizungumza jana,
Mratibu wa soka la ufukweni, Deogratius Lucas alisema baada ya kukamilika kwa ligi ya
taasisi Desemba itaanza ligi ya klabu.
"Shirikisho
linavitaarifu vyuo na taasisi za elimu ya juu kuchukua fomu za usajili wa timu
zao kwa ajili ya kushiriki ligi hiyo," alisema Lucas.
Pia Lucas alisema
fomu zinapatikana katika ofisi za TFF na kwamba mwisho wa kuchukua ni Novemba
6.
"Serikali za
wanafunzi kupitia wizara ya michezo wanatakiwa kufika kuchukua fomu kwa ajili
ya kujisajili ikiwa ni pamoja na kuthibitisha ushiriki wao", alisema
Lucas.
Aidha Lucas alisema
timu zote za mpira wa miguu wa ufukweni za mtaani zinatakiwa kujisajili kwa
ajili ya ligi yao ambayo itaanza mwishoni mwa Desemba. Kwa ukanda wa Afrika Mashariki Tanzania
inashika nafasi ya kwanza pamoja na Kenya na Uganda katika ubora na kwa Afrika
inashika nafasi ya 12.
No comments:
Post a Comment