Michuano ya
Kombe la Shirikisho la Azam ‘Azam Sports Federation Cup ‘(ASFC), imezinduliwa
rasmi leo kwa droo maalumu kwa timu
zitakazofungua dimba kwa mzunguko wa awali.
Akizungumza Mkurugenzi
wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi alisema ligi hiyo itashirikisha timu 91 na itaanzia
hatua ya awali kabla ya kuja kwa raundi ya kwanza.
“Azam
federation Cup itashirikisha timu 91 ambapo timu 16 ni za Ligi Kuu, 24 za Ligi
Daraja la Kwanza, 24 za Ligi Daraja la Pili na 27 za Ligi ya Mabingwa wa Mkoa ,”
alisema Madadi.
Hatua ya
awali itashirikisha kundi la timu 27 za mabingwa wa mikoa timu sita
zitakazocheza mechi tatu na baada ya wachezaji watatu wa zamani wa timu ya
taifa Abeid Mziba , Boniface Pawasa na Salum Sued kuchagua vitufe sita kupata
timu hizo.
Timu
zilizopatikana katika droo hiyo hatua ya awali Buselesele ya Geita itayocheza
na Green FC ya Songwe, Kisarawe United ya Pwani itacheza na Silabu ya Mtwara
wakati Usamala ya Simiyu itacheza na Sahale All Stars ya Tanga kati ya Oktoba
31, Novemba Mosi au mbili.
Raundi ya
Kwanza itaanza Novemba 7, 8 au 9 na timu zilizochaguliwa kwenye droo hiyo ni Mashujaa
ya Kigoma itacheza na Mshindi kati ya Buselesele ya Geita na Green FC ya Songwe,
wakati mechi nyingine zitakuwa Msange ya Tabora itacheza na Milambo pia ya
Tabora na Bulyanhulu ya Shinyanga itacheza na Area C ya Dodoma.
Mji Mkuu FC
ya Dodoma imeangukia kwa Nyundo ya Kigoma wakati Baruti FC ya Mara itacheza na
Ambassodor ya Kahama, Shinyanga huku Eleven Stars ya Kagera ikipangwa kucheza
na Ndovu ya Mwanza.
Changanyikeni
ya Dar es Salaam itacheza na Reha FC pia ya Dar es Salaam wakati Mshindi kati
ya Kisarawe United na Silabu ya Mtwara atacheza na Kariakoo ya Lindi huku
Cosmopolitan ikicheza na Ajabalo wakati Makumba FC itapambana na Green Warriors
ya Kinondoni wakati Namungo FC ya Lindi itachuana na Villa Squad ya Dar es
Salaam huku Dar City ikicheza na Majimaji Rangers ua Nachingwea.
Michezo
mingine ya hatua ya kwanza itakutanisha timu za Shupavu FC ya Morogoro na
Sabasaba pia ya mjini humo wakati Motochini FC ya Katavi dhidi ya Ihefu FC ya
Mbeya wakati The Mighty Elephant ya itacheza na Makanyagio ya Rukwa.
Timu ya
Burkina FC ya Morogoro itacheza na Mbinga United ya Ruvuma wakati Makambako
Heroes ya Njombe itacheza na Mkamba Rangers ya Morogoro wakati Real Moja
Moja itapambana na African Wonderers – zote za Iringa. Boma FC ya Mbeya
itacheza na African Sports ya Tanga.
Mechi
nyingine za hatua hiyo itakuwa ni kati ya Pepsi ya Arusha ambayo itacheza na
Kilimanjaro Heroes ya Kilimanjaro; huku Stand Misuna ya Singida itacheza na
Madini FC ya Arusha ilihali AFC ya Arusha itacheza na Nyanza ya Manyara wakati
New Generation itacheza na Mshindi kati ya Usamala FC na Sahale ya Tanga.
Bodaboda FC itacheza na Kitayose ya Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment