SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) limesema halitasitisha mchakato wa Uchaguzi Mkuu licha
ya kupokea barua ya zuio kutoka Baraza la Michezo Tanzania (BMT)
Akizungumza
na wandishi wa habari jana, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine alikiri kupokea
barua ya BMT na kusema wamewaandikia kukutana nao mapema.
“Tunatarajia
kukutana nao maana namini wanafanya hivi kwa sababu ya afya ya mpira wa miguu
lakini hatutasimamisha uchaguzi kwa sababu utakuwa nje ya katiba,” alisema Selestine.
Selestine
alisema katiba ya TFF inawakata uchaguzi kufanyika kabla ya Agosti kumalizika
hivyo wakisitisha mchakato watakuwa wanakiuka katiba.
“Uchaguzi
Mkuu wa TFF ni agenda moja tu katika mkutano huo hivyo ukisitisha mchakato wa
uchaguzi unaweza kujikuta umefika mwakani bila uchaguzi kufanya pia kamati
inayosimamia uchaguzi ipo kihalali kulingana na katiba ya TFF,” alisema
Selestine.
Juni 13
Baraza la Michezo lilimwandikia barua kwa Katibu Mkuu wa TFF kutaka kusitishwa
kwa uchaguzi wa viongozi wakuu wa TFF kwa sababu halijajulishwa kuwepo kwa
uchaguzi huo.
Pia barua
hiyo iliwataarifu TFF kuwa kamati ya nidhamu, rufaa na usuluhishi ya Baraza
inataka kukutana na kamati ya itendaji ya TFF Julai Mosi saa nne asubuhi katika
ofisi za baraza zilizopo Uwanja wa Taifa.
Lakini pia
Selestine alisema wao wana katiba yao inayojitegemea na wanapaswa kuwasilisha
BMT matokeo ya uchaguzi lakini siyo kuwajulisha juu ya mchakato wa uchaguzi.
Wakati huo
huo, Mjumbe wa kamati ya utendaji ya TFF anayewakilisha kanda ya Tabora na
Kigoma, Alhaji Ahmed Mgoyi ametangaza kutogombea nafasi yoyote katika uchaguzi
ujao.
Alhaji Mgoyi
amekuwa mjumbe wa Kamati ya utendaji kwa muda mrefu (2004-2017) kuanzia enzi za
utawala wa Leodgar Tenga hadi sasa kwenye uongozi wa Jamal Malinzi.
Katika
waraka wake aliotoa katika vyombo vya habari Alhaj Mgoyi alisema ameamua kwa
ridhaa yake ili kutoa fursa kwa wengine kugombea na kuomba radhi kwa watu ambao
hawakutarajia kuona akitoa uamuzi huo.
No comments:
Post a Comment