WACHEZAJI wa
Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta na Farid Mussa wameachwa katika kikosi
kinachokwenda kushindana kuwania mashindano yanaandaliwa na Baraza la soka la
nchi za Kusini mwa Afrika (COSAFA) nchini Afrika Kusini
Katika
kikosi hicho Kocha Salum Mayanga ametangaza wachezaji 22 ambao watashiriki
Kombe la Castle Cosafa nchini Afrika Kusini yanayotarajiwa kuanza Juni 25 na
wataingia kambini Jumapili ya wiki hii.
Katika safu
ya ushambuliaji Mayanga ameongeza , Stamil Mbonde, Elius Maguli ambao wanacheza
soka Oman katika klabu ya Dhofar SC na kuwaacha Mbwana Samatta, Ibrahim Ajib na
Abdulrahman Mussa.
Kadhalika
katika nafasi ya viungo washambuliaji ameawaacha, Jonas Mkude, Salum Abobakar
‘Sure Boy’ na Farid Mussa na kumwongeza Rapahel Daudi kutoka Mbeya City ambaye
atasaidiana na Mzamiru
Yassin, Simon Msuva na Shizza Kichuya.
Akizungumza
kocha Mayanga alisema anaamini kikosi hicho kitakwenda kutetea bendera ya
Tanzania katika mashindano japo wanashiriki kama mwaliko.
“Nimelazimika
kutumia wachezaji wengi wanaocheza ligi ya ndani kwani baada ya COSAFA Julai
tutakuwa na mchezo wa kuwania kufuzu mashindano ya Afrika kwa wachezaji
wanaocheza ndani (CHAN) hivyo watakuwa wamepata maandalizi,” alisema Mayanga.
Kikosi hicho
kinaundwa na makipa Aishi Manula (Azam FC), Benno David Kakolanya
(Yanga) na Said Mohammed Said (Mtibwa Sugar).
Walinzi wa
pembeni upande wa kulia ni Shomari Kapombe (Azam FC) na Hassan Ramadhan
‘Kessy’ (Yanga) wakati upande wa kushoto wapo Gadiel Michael (Azam FC) na Amim
Abdulkarim (Toto Africans).
Walinzi wa
kati ni Erasto Nyoni (Azam FC), Salim Abdallah (Mtibwa Sugar), Abdi Banda
(Simba) na Nurdin Chona (Tanzania Prisons) wakati viungo wa kuzuia kuwa ni
Himid Mao (Azam FC) na Salmin Hoza (Mbao FC).
Viungo
washambulia ni Mzamiru Yassin (Simba), Simon Msuva (Yanga), Raphael Daudi
(Mbeya City) na Shizza Kichuya (Simba).
Washambuliaji
ni Thomas Emmanuel Ulimwengu (AFC Eskilstuna – Sweden), Mbaraka Yusufu (Kagera
Sugar), Stamili Mbonde, Elius Maguli (Dhofar SC) na Shabani Idd Chilunda (Azam
FC).
Tanzania
imepangwa kundi A ambako wapinzani wake ni Mauritius, Malawi na Angola wakati
Kundi B ni Msumbiji, Shelisheli, Madagascar na Zimbabwe.
Tanzania
itacheza mchezo wa kwanza dhidi ya Malawi Juni 25 kabla ya kukutana na Angola
Juni 27 na kumaliza hatua ya makundi Juni 29 kwa kucheza na Mauritius.
Timu za
Botswana, Zambia na Afrika Kusini, Namibia, Lesotho na Swaziland zitakuwa na
mechi maalumu ya mtoano (play off) ili kuingia robo fainali ya mashindano haya
ambayo yalianzishwa 1997 na
yatashirikisha timu 14
No comments:
Post a Comment