MGOMBEA wa
Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Athumani Nyamlani
amejitoa kwenye kinyang’anyiro katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika
Agosti 12 mwaka huu mjini Dodoma.
Nyamlani
ambaye amewahi kuwa Makamu wa Rais wa TFF aliwasilisha
barua jana ikiwa ni siku moja tu tangu Kamati ya Uchaguzi ipitishe jina lake
kuwa miongoni mwa wagombea 10 wanaowania nafasi hiyo kwa sababu ni masuala
binafsi.
Akizungumza
na gazeti hili, Ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas alisema baada ya Nyamlani
kujiaondoa wagombea wanaobaki tisa kwenye kinyang’anyiro ambao watahitajika
kufika kwenye usaili Juni 29.
“Baada
ya Nyamlani kujiondoa sasa wagombea wanaobaki ni Jamal Malinzi, Imani Madega,
Wallace Karia, Fredrick Masolwa, Fredrick Mwakalebela, John Kijumbe, Shija
Richard, Ally Mayay na Emmanuel Kimbe,” alisema Lucas.
Mbali
na Nyamlani kujitoa, mgombea wa nafasi ya Kamati ya Utendaji TFF, kutoka kanda ya
Kagera na Geita, Abdallah Mussa aliondolewa kwa sababu ya kutoambatanisha
kivuli cha cheti ya elimu ya sekondari.
Jumla
ya wagombea 74 waliomba kuwania nafasi mbalimbali hivyo sasa wamebaki wagombea
72, urais ukiwa na wagombea tisa, Makamu wa Rais sita na wajumbe wa kamati ya
utendaji 58.
Wakati huo
huo kamati ya Uchaguzi ya TFF imesema uchaguzi wa klabu ya
Lipuli ya Iringa utafanyika Agosti 5, na utasimamiwa na kamati hiyo.
Awali uchaguzi huo ulikuwa ufanyike Mei 29 lakini baada ya
kamati kufuatilia taratibu mbalimbali, kanuni na sheria na kujirisha sasa
mchakato huo utaanza kesho.
Tayari Kamati ya Uchaguzi ya TFF iko Iringa kwa ajili ya
kutangaza rasmi uchaguzi huo ambako zoezi la kuchukua na kurejesha fomu
litaanza Juni 28, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment