TAASISI ya kulinda wanyama pori ya WildAid leo
imekabidhi vifaa kwa Shirikisho la SokaTanzania (TFF) baada ya jana kuingia
makubaliano ya kushirikiana.
Juzi Rais wa
TFF, Jamal Malinzi aliingia makubaliano na WildAid ya kushirikiana kupinga
ujangili kupitia timu ya Taifa ya Vijana miaka 17, ‘Serengeti Boys’.
Akizungumza
baada ya kupokea vifaa hivyo, Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa alishukuru WildAid kwa
msaada huo na kusema umekuja wakati muafaka.
“Vijana wetu
wetu wanaweza kuvaa fulana hizi wakati wa kupasha mwili joto katika mashindano
ya Afrika pia wadau wa michezo watavaa kuonesha kuwa wanapinga ujangili,’
alisema Mwesigwa.
Naye Mshauri
wa WildAid Tanzania, Lily Massa alisema wanafurahi kufanya kazi na TFF kwa
sababu kupitia mchezo wa soka unapendwa na watu wengi ujumbe wao utawafikia
watu wengi.
“Nafurahi
kufanya kazi na TFF kwani inabeba idadi kubwa ya watu kwa wakati mmoja hivyo
elimu kuhusu ujangili na utunzaji wa wanyama pori na mazingira itafika kwa
jamii,” alisema Lily
WildAid
tayari inafanya kazi na mchezaji nyota wa mpira wa kikapu, Hasheem Thabeet
anayecheza Marekani na mwanamuziki Ali Kiba, BenPal na mfanyabiashara Mohamed
Dewj ‘MO’ hivyo kuongezeka kwa TFF kunafanya wafikie watu wengi.
|
Friday, May 5, 2017
WILDAID YAFANYA KWELI KWA SERENGETI BOYS LEO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment