WENYEJI wa
taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, ‘Serengeti Boys’ timu ya Cameroon
juzi walilipiza kisasi cha kufungwa bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki
uliochezwa mjini Yaounde, Cameroon.
Awali Aprili 30, Serengeti boys iliifunga Cameroon 1-0 katika mchezo mwingine wa kujipima nguvu. Akizungumza na gazeti hili Kocha Mkuu wa Serengeti boys, Bakari Shime alisema katika mchezo huo licha ya kufungwa walicheza vizuri.
“Soka ni
mchezo wa makosa, wenzetu waliingia wakiwa wamekamia kulipa kisasi lakini
pamoja na kupoteza mchezo, wachezaji walicheza vizuri,” alisema Shime maarufu
kama mchawi mweusi.
Pia Shime
alisema huo ndio mchezo wa mwisho wa kirafiki zaidi watakuwa wanaendelea na
programu za mazoezi ya kawaida.
Serengeti
Boys ipo Younde, Cameroon tangu wiki iliyopita ikitokea Morocco ambako iliweka
kambi na kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Gabon na kushinda 2-1 kila
mchezo.
Serengeti
boys inarajiwa kuwasili Gabon Mei 7 ambako imepangwa kundi B pamoja na timu za
Mali, Niger na Angola na Cameroon imepangwa kundi A lenye timu za wenyeji,
Gabon, Guinea na Ghana.
Itafungua
dimba na bingwa mtetezi Mali Mei 15 mjini Libreville Gabon ambako kundi B
litakuwa likicheza.
|
Thursday, May 4, 2017
SERENGETI BOYS YAKWAA KISIKI CAMEROON
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment