SHIRIKA la
Kimataifa la kulinda wanyamapori la WildAid limeingia makubaliano na Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) kwa ajili ya kuifadhili timu ya Taifa ya Vijana miaka 17,
‘Serengeti Boys’.
Akizungumza
wakati wa kuweka saini makubaliano hayo Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) Jamal Malinzi alisema wamefurahi kufanya kazi za kijamii hasa hii ya
kupiga vita ujangili dhidi ya wanyama pori.
“Utunzaji mbaya wa mazingira unafanya wanyama
kukimbia maeneo yao ya asili na ujangili unamaliza wanyama hasa Tembo hivyo
kupitia Serengeti boys tutakuwa na nafasi ya kueleimisha jamii juu ya kuifadhi
wanyama na mazingira kwa ajili ya vizazi vijavyo,” alisema Malinzi.
Upande wa
jamii tunapenda kushirikiana na jamii kwa ajili ya kufikisha ujumbe kwa jamii
huku akitolea mfano kick aids na kujikinga na malaria ambayo ilitekelezwa
kipindi cha Tenga.
Naye Mshauri
wa WildAid Tanzania Lily Massa alisema anashukuru kufanya kazi na TFF kwa
sababu mchezo wa soka unapendwa na watu wengi hivyo watakuwa wanaelimisha
umuhimu wa WildAid.
“Nafurahi
kufanya kazi na TFF kwani unabeba idadi kuwa ya watu kwa wakati mmoja hivyo
elimu kuhusu ujangili na utunzani wa wanyama pori na mazingira itafika kwa
jamii,” alisema Lily
WildAid
tayari inafanya kazi na mchezaji nyota wa mpira wa kikapu, Hasheem Thabeet
anayecheza Marekani na mwanamuziki Ali Kiba, BenPal na mfanyabiashara Mohamed
Dewj ‘MO’ hivyo kuongezeka kwa TFF kunafanya wafikie watu wengi.
No comments:
Post a Comment