Monday, May 1, 2017
NMB WATEMBELEA AZAM COMPLEX
WADHAMINI wakuu wa klabu ya Azam FC, Benki ya NMB hivi karibuni ilifanya ziara katika makao makuu ya timu hiyo ‘Azam Complex’ na kushuhudia maendeleo mbalimbali yanayotokana na uwekezaji huo.
Akizungumza na gazeti hili Meneja wa kikosi cha Azam FC Philipo Arando, aliwashukuru NMB, kwa udhamini wao ambao umekuwa chachu kubwa ya mafanikio waliyokuwa nayo tangu walipoanza kufanya nao kazi mwaka wa tatu sasa.
"Ukweli mafanikio yetu Azam FC, yanatokana na udhamini mnono kutoka kwa NMB katika kipindi cha miaka mitatu tukiwa chini yao tumeweza kufanya vizuri kwenye ligi ya Vodacom kwa kumaliza nafasi ya pili mara mbili na kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho, lakini pia tumeweza kuwa mabingwa wa Kombe la Kagame jambo ambalo tunajivunia sana licha ya uchanga wetu," alisema Arando.
Meneja huyo alisema baada ya kumudu ushindani wa ligi ya ndani mikakati yao ni kuhakikisha wanajenga timu imara itakayocheza fainali za Afrika kwa miaka ijayo.
Aidha ziara hiyo iliwapa fursa wafanyakazi wa NMB, kuzungumza na wachezaji nyota wa Azam ili kujua mambo mbalimbali kutoka kwao na waliweza kujifunza mengi ikiwemo sababu ya timu hiyo kuanza vibaya ligi ya msimu huu.
Baada ya ziara hiyo timu ya soka inayoundwa na wafanyakazi wa NMB ilicheza mechi ya kirafiki na timu ya vijana U-20 ya Azam na baada ya dakika 90 wadhamini walipoteza mchezo kwa kipigo cha mabao 7-2.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment