BENDI za
Sikinde na Msondo Ngoma zitafanya onyesho la pamoja Mei 20 katika Ukumbi wa
Traventine Magomeni kumaliza ubishi nani mkali zaidi ya mwenzake.
Akizungumza
wandishi wa habari leo, Abdulfareed Hussein alisema kuwa mpambano huo mshindi
ataamuliwa na mashabiki baada kimya cha miaka miwili mara ya mwisho kupambana.
“Mshindi
ataamuliwa na mashabiki ambao watakuwepo ukumbini siku hiyo na kukabidhiwa
zawadi ambayo itatangazwa hapo ukumbini siku hiyo,” alisema Hussein.
Pia Hussein
alisema wanaamini lengo la kuandaa pambano hilo dhidi ya bendi hizo kongwe za
muziki wa dansi ambazo ni hasimu ni kutoa burudani na kukuza muziki wa dansi.
Akizungumza
juu ya pambano hilo Meneja wa Msondo Ngoma, Said Kibiriti alisema watanzania
wajiandae kupata burudani kuanzia enzi za NUTA, JUWATA na OTTU ili wale vijana
wa zamani wakumbuke enzi zao.
“Sisi kambi
yetu itakuwa Pemba Wete na tukirudi hapa wale vijana wa zamani na wa sasa
wajiandae kupata burudani ya ukweli katika ukumbi wa Traventine,” alisema
Kibiriti
Naye
kiongozi wa Sikinde Abdallah Hema alijigamba kuhakikisha wanatoa buradani isiyo
na kifani
No comments:
Post a Comment