wakwanza kushoto ni muaandaji wa
bonanza la Afya kwanza akiwa na timu ya Triple a klabu Fc kabla
ya mechi kuanza(habari picha na Woinde Shizza wa
libeneke la kaskazini )
timu ya tigo Fc ikiwa pamoja na timu
ya Triple A klabu FC
timu ya mringa ringa
iikiendelea kufanya mazoezi kabla ya kuingia
uwanjani
timu ya wavuta kamba ikiendelea
kuvuta kamba
warembo wakifuatilia mpira kwa
makini
timu ya Triple A wakiwa
wanapeana mawazo katika kipindi cha mapunziko
wadau mbalimbali waliouthuria
bonanza hilo wakiendelea kupata vinywaji
mmoja ya wachezaji wa timu ya
Triple A klabu Fc akiwa anatolewa uwanjani na wauguzi mara baada
yakuumia wakati akicheza
Timu ya Tigo Fc ikiwa katika picha ya
pamoja kabla ya mechi baina yao na timu ya Triple A Klabu Fc kuanza
Na Woinde
Shizza,Arusha
Timu ya
Triple A klabu imelazimika kutoka sara ya bao moja
kwa moja na timu ya Tigo FC katika
bonanza la michezo lijulikanalo kwa jina la Afya Kwanza
lililofanyika katika viwanja vya Gymkana
jijini hapa
Bonanza
hilo ambalo
ni mara ya kwanza kufanyika limeandaliwa na
mkurugenzi wa Bendi ya Rickernest music band ,bendi ambayo makao makuu
yake ni jijini hapa na imeshirikisha michezo mbalimbali ikiwemo kuvuta
kamba pamoja na mpira wa miguu
Akiongelea
bonaza hilo muandaaji wa mashindano hayo
Denis Mtedeki alisema
kuwa nia rasmi ya kuandaa bonanza hili ni kuwakutanisha watu
mbalimbali na kufurahi pamoja pamoja na kushiriki michezo
,ikiwa kama ni sehemu ya kufanya
mazoezi
Alisema kuwa
bonanza
hili limeshirikisha jumla ya timu za mipira wa miguu mbili pamoja na timu
zingine mbili ambazo zilifanya kazi ya kuvuta kamba,alizitaja timu hizo kuwa ni
timu kutoka kampuni ya simu ya Tigo
(Tigo Fc), Olemringaringa FC, Red Apple,Mijada Fc pamoja na
Triple a klabu FC.
Denis
aliongeza kuwa
mbali na kushiriki bonanza hili pia wachezaji na washiriki waliouthuria
walipata fursa ya kupima magonjwa mbalimbali ikiwemo kupima presha na kisukari
bure.
Aidha
aliongeza kuwa bonanza hili alitaishia hapa bali
litakuwa likifanyika kila mwisho wa mwezi lengo ikiwa ni kufanya mazoezi
,kuwakutanisha wadau mbambali mbali na kufurahi pamoja
No comments:
Post a Comment