KOCHA wa African Lyon, Charles Otieno
amejigamba kuifunga Mbao FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu utakaochezwa kesho kwenye
Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Akizungumza kwa njia ya simu, Otieno alisema anajua Mbao ni timu nzuri lakini pia wao ni
wavuri ndio maana wanacheza ligi kuu hivyo anatarajia kurudi na pointi tatu.
“Naijua
Mbao FC ni timu nzuri na watacheza nyumbani na kuongezewa nguvu na mashabiki
wao lakini maandalizi ambayo nimefanya kipindi cha wiki mbili yananipa jeuri ya
kusema nitachukua pointi tatu ugenini,” alisema Otieno
Mchezo huu
unatarajiwa kuwa na ushindani kwani timu hizi zimeachana kwa pointi moja,
African Lyon inashika nafasi ya 11 ikiwa na pointi 20 na Mbao wana pointi 19
kwenye nafasi ya 12.
Ligi Kuu
inatarajia kuendelea Januari 16, 2017 ambapo Tanzania Prisons itakuwa mgeni wa
Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Januari 17, 2017, Majimaji ya Songea
itakuwa wenyeji wa mabingwa watetezi Yanga katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa
Majimaji mkoani Ruvuma.
Mtibwa Sugar itakacheza na Simba,
Januari 18, 2017 kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro wakati Azam itakuwa mwenyeji
wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Mchezo wa Azam na Mbeya City utaanza
saa 1.00 usiku lakini michezo mingine itaanza saa 10.00 jioni lengo likiwa ni
kutoa nafasi kwa mashabiki kushuhudia mechi nyingi kupitia Kituo cha
Televisheni cha Azam ambao ni wadhamini
wenza wa ligi kuu.
No comments:
Post a Comment