Limekuwa
jambo la kawaida kuwasikia watani wa jadi Simba na Yanga kufanya mambo
ambayo mpinzani mmoja anakuwa anafanya na sasa linalosubiriwa kwa hamu
ni kuona kama Yanga watawaiga Simba baada ya wao kukubaliana
kufanya mabadiliko ya mfumo ambao wanautumia sasa.
Akizungumza
na waandishi wa habari kuelekea mkutano wa Yanga ambao umeitishwa kwa
dharula na mwenyekiti wa timu, Mratibu wa matawi ya Yanga na Mkuu wa
Kitengo cha Masoko wa Yanga, Omary Kaaya alisema jambo hilo linauwezekano
wa kujadiliwa katika mkutano wa kesho ila tu endapo mwenyekiti atataka
kulizungumzia.
“Kama
tumevyosikia majirani nzetu kuna wenzetu kuna mtu anataka kuwekeza ili
kuona kama wanaweza kupata mafanikio baada ya kuona sisi tunakuwa na
mafanikio na kweli hilo ni jambo ambalo linahitaji kufanyiwa mabadiliko
ya kimfumo,
“Kama
kutakuwa na maoni ya wanachama ambao wanataka na sisi kuwepo na mtu
ambaye anataka kufanya kama MO anavyotaka kufanya kwa Simba basi
mwenyekiti atalizungumzia hilo maana imeshakuwa kawaida jirani akifanya
jambo mwingine na yeye analifanya,” alisema Kaaya.
Aidha
Kaaya alizitaja ajenda za mkutano wa kesho kuwa ni 1.Mwenendo wa
Timu, 2.Mahusiano kati ya Yanga na TFF, 3.Katiba ya Yanga, 4.Mapato
na Matumizi ya Klabu, 5.Shukrani kwa Wajumbe waliomaliza muda
wao, 6.Kuishukuru Serikali kwa ushirikiano wanaonyesha kwenye mashindano
tunayoshiriki, 7.Maendeleo ya klabu na 8.Mengineyo.
Pia
katika hatua nyingine Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari wa
Yanga, Jerry Muro amesema kuwa amerejea kazini kuendelea na kazi baada
ya kumaliza likizo yake na kutuma ujumbe kwa TFF kuwa amepata barua yao
lakini bado anahitaji barua ya hukumu.
“Niombe
kupta nakala ya hukumu tuisome na tujue wametumia sheria gani na kanuni
gani ambazo wametumia kunihukumu na baada ya hapo tutaangalia kama
tunakata rufaa au tunaacha kwahiyo niwatumie taarifa ndugu zangu wa TFF
kuwa wajue nimerudi,” alisema Muro.
No comments:
Post a Comment