Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, July 20, 2016

LIGI KUU ENGLAND: UHAMISHO WA WACHEZAJI WAPYA

UHAMISHO wa Wachezaji na Klabu kununua Wachezaji Wapya umeshika hatamu katika Kipindi hiki cha Dirisha la Uhamisho ambalo litafungwa Agosti 31.
Kwa Klabu za Ligi Kuu England, Bournemouth inaongoza kwa kuwa na Wapya 7 lakini Sunderland na Stoke City hadi sasa hazina mpya hata mmoja.
PATA TAARIFA KWA KILA KLABU:
-Bournemouth, Mtu 7, Emerson Hyndman wa Fulham, Nathan Ake wa Chelsea kwa Mkopo, Lys Mousset wa Le Havre, Mark Travers kwa Mjaribio, Mikael Ndjoli toka Millwall, Lewis Cook wa Leeds na Jordon Ibe toka Liverpool.

-West Ham, Mtu 6, Toni Martinez wa Valencia kwa Pauni Milioni 2.4, Havard Nordveit wa Borussia Monchengladbach, Domingos Quina, Sofiane Feghouli wa Valencia, Gokhan Tore wa Besiktas kwa Mkopo, Ashley Fletcher wa Man United, Bure bila Ada.

-Middlesbrough,
Mtu 6, Viktor Fischer wa Ajax kwa Pauni Milioni 3.8, Bernado Espinosa wa Sporting Gijon, Marten De Roon wa Atalanta kwa Pauni Milioni 12, Jordan Mc Ghee wa Heart of Midlothian kwa Mkopo, Victor Valdes toka Man United, Ada ni Bure, Antonio Barragan wa Valencia kwa Pauni Milioni 3.

-Leicester City, Watano, Ron-Robert Zieler wa Hannover 96, Luis Hernandez wa Sporting Gijon, Raul Uche Rabio wa Valencia, Nampalys Mendy wa Nice na Ahmed Musa wa CSKA Moscow kwa Pauni Milioni 18.

-Watford, Wanne, Jerome Sinclair toka Liverpool, Pauni Milioni 4, Christian KAbasele wa Genk, Isaac Success wa Granada na Juan Camilo Zuniga, Mkopo kutoka Napoli.

-Everton, Watatu, Bassala Sambou wa Coventry City, Chris Renshaw wa Oldham Athletics na Maarten Stekelenburg wa Fulham.

-Swansea City, Watatu, Leroy Fer wa QPR, Pauni Milioni 3, Mike van der Hoorn wa Ajax na Tyler Reid wa Man United.

-Man United, Watatu, Eric Bailly kutoka Villareal, Pauni Milioni 30, Zlatan Ibrahimovic na Henrikh Mkhitaryan kutoka Borussia Dortmund.

-Man City, Watatu, Ilkay Gundogan kutoka Borussia Dortmund, Pauni Milioni 21, Nolito toka Celta Vigo, Pauni Milioni 14 na Oleksandr Zinchenko toka FC Ufa.

-Liverpool ni watatu, Joel Matip wa Schalke, Loris Karius waMainz kwa Pauni Milioni 4.7 na Sadio Mane toka Southampton kwa Pauni Milioni 34.

-Crystal Palace ni watatu ambao ni Andros Townsend, toka Newcastle, Pauni Milioni 13, Steve Mandanda toka Marseille na James Tomkins wa West Ham kwa Pauni Milioni 10.

-Tottenham ni Wawili, Victor Wanyama kutoka Southampton, Pauni Milioni 11, na Vincent Janssen toka AZ Alkmaar kwa Pauni Milioni 17.
-Arsenal Wawili Granit Xhaka kutoka Borussia Monchenglabach, Pauni Milioni 35 na Takuma Asano kutoka Hiroshima Sanfrecce.

-Chelsea imewasaini Michy Batshuayi kutoka Marseille kwa Pauni Milioni 33 na N’Golo Kante kutoka Leicester City kwa Pauni Milioni 30.

-Southampton,
Wawili, Nathan Redmond kutoka Norwich City na Pierre-Emile Hojbjerg kutoka Bayern Munich kwa Pauni Milioni 12.8

-Burnley, Mcheza mmoja, Jimmy Dunne, Uhamisho wa Bure

-Hull City imesaini mmoja, Will Mannion kutoka AFC Wimbledon, Ada haijaamuliwa.

-WBA imesaini mmoja kutoka QPR, Matt Phillips, kwa Ada ambayo haikutajwa.

-Sunderland haijasaini Mchezaji

-Stoke City pia haina mpya

No comments:

Post a Comment