RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Jamal Malinzi ameupongeza uongozi mpya wa Chama cha Soka Mkoa wa Dodoma
ulioingia madarakani Jumamosi Julai 16, 2016.
Akizungumza na wandishi wa habari, Malinzi alisema
viongozi waliofanikiwa kuingia madaraka wana kazi ya kusimamia soka na
kuhakikisha kanuni na sheria za soka zinafuatwa ili kuleta maendeleo na kuondoa
malumbano.
“Nawapongeza wote waliochaguliwa kuongoza DOREFA ila
wajue kuwa uongozi ni dhamana hivyo wana Dodoma wanatarajia kuona soka
linachezwa bila kuwa na migogoro”, alisema Malinzi
Waliofanikiwa
kuingia madarakani ni Mulamu Nghambi aliyeshinda nafasi ya Uenyekiti kwa kupata
kura zote 27 wakati Makamu Mwenyekiti ni Geofrey Ngolly aliyepata kupata 25.
Katibu Mkuu ni Mussa Kissoy aliyevuna kura 19 kwa
kumshinda Abubakar Ibrahim aliyepata kura nane na Katibu Msaidizi ni Abdallah
Ibrahim aliyeshinda kwa kura zote 27.
Dickson Kimaro alishinda nafasi ya Mjumbe wa Mkutano
Mkuu wa TFF na Mwakilishi wa klabu mbalimbali ikichukuliwa na Mohammed Aden na
wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Esther Ntomola,
Morice Sarara na Lister Manyara
@@@@@@@@@@@@@@@@@
Na Rahel Pallangyo
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linatarajia
kutoa madawati 200 ikiwa ni sehemu ya mapato ya Ngao ya Hisani utakaochezwa
Agosti 17, 2016.
Akizungumza na wandishi wa habari, Afisa habari wa
TFF, Alferd Lucas, alisemna TFF inaunga mkono juhudi za Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na juhudi za Serikali kwa katika kuhakikisha vijana wa
Kitanzania wanakuwa na mazingira bora ya kupata elimu.
“TFF imeona umuhimu wa kusaidia elimu ya Tanzania ndio
maana imeamua
kutoa sehemu ya mapato yake kama mchango wa kusaidia
madawati kupitia mchezo wa ngao ya jamii utakaochezwa Agosti 17 kuashiria msimu
mpya wa Ligi Kuu”, alisema Lucas.
Pia Lucas alisema TFF inamshukuru Katibu Mkuu wa Bunge, Dkt.
Thomas Kashililah kwa juhudi za kuendelezaa mpira wa miguu na kuutumia katika
kuliletea Taifa maendeleo.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania litaendelea
kushirikiana na Ofisi ya Bunge Sports Club katika kufanikisha mashindano
mbalimbali hasa mchezo wa Hisani kati ya Simba Sports Club na Young African
(Wabunge) utakaofanyika hapo baadaye kwa mujibu wa ratiba na uratibu wa Bunge.
Mchezo wa Ngao ya Jamii utazikutanisha Yanga na Azam
FC na utachezwa Agosti 17 kwenye Uwanja wa Taifa kuashiria msimu mpya wa Ligi
Kuu Tanzania Bara.
No comments:
Post a Comment