Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, March 3, 2016

WENGER HOFU TELE, PAUL SCHOLES AWAPONDA

BAADA ya Jana kutandikwa 2-1 na Swansea City ikiwa ni kipigo chao cha pili mfululizo kwenye Ligi Kuu England, Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amekiri kupatwa na wasiwasi.
Jumapili iliyopita Arsenal ilipigwa 3-2 na Man United huko Old Trafford na Jana wakiwa kwao Emirates wengi walitegemea kuwa Arsenal itamaliza hasira zao kwa Swansea lakini wakajikuta wakipigwa 2-1 licha ya wao kutangulia kufunga.Baada ya kipigo hicho, Wenger alisema: "Kwa sasa nina wasiwasi na matokeo. Lazima tukae chini na kujifua. Wachezaji wamevunjwa moyo lakini inabidi turejee!"
Nae Paul Scholes, Mchezaji wa zamani wa Man United ambae sasa ni Mchambuzi kwenye TV, amesema ile imani yake kuwa Arsenal Msimu huu itatwaa Ubingwa baada ya kuukosa Miaka 12 sasa imetoweka.
Scholes ameeleza kwenye BT Sport: "Msimu huu Arsenal imenihadaa. Nilidhani Msimu huu wamejengeka lakini wametudanganya. Kama kawaida kwenye hatua muhimu za mwisho Arsenal imekumbwa na kiwewe, imesambaratika!"
Aliongeza: "Wameshindwa kupata matokeo Gemu kubwa na muhimu na nadhani mwishoni mwa Msimu kama Wenger hapati Ubingwa atakuwa na presha kubwa!"
Kipigo hicho cha Swansea kimewaacha Arsenal Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 6 nyuma ya Vinara Leicester City na Pointi 3 nyuma ya Timu ya Pili Tottenham ambayo Jumamosi hii wanaifuata huko White Hart Lane kucheza nayo.

Nacho Monreal

Kevin Quigley

Kipa Cech

No comments:

Post a Comment