Ben Pol, Country Wizzy na Magwiji wa Afrika Kusini Kutikisa TFSA 2025!

 



Tanzania – Desemba 20, 2025, jijini Dar es Salaam patakuwa kitovu cha urembo, ubunifu, na burudani wakati tukio kubwa la Tanzania Fashion & Style Awards (TFSA) litakapofanyika. 

Mwaka huu, jukwaa la mitindo linakutana na ladha ya kipekee ya muziki wa R&B na HipHop, huku kukiwa na mwaliko wa kipekee kwa magwiji (Gurus) wa mitindo kutoka Afrika Kusini.

Katika kunogesha usiku huo wa tuzo, mfalme wa R&B Afrika Mashariki, Ben Pol, atapanda jukwaani kuleta "New Experience". Ben Pol, ambaye anatamba na albamu yake mpya ya ‘Flamingo’ (inayoelezwa kuwa darasa la maisha na mapenzi), atashusha burudani itakayooana na miondoko ya Runway.

Si yeye tu, mkali wa HipHop anayetikisa kwa sasa, Country Wizzy, naye amethibitishwa kuwepo. Hii ni "Fashion meets HipHop," ambapo weledi wa mitindo unakutana na nguvu ya muziki wa kizazi kipya.

TFSA 2025 si tukio la kawaida; ni sherehe ya kutathmini na kuenzi kukua kwa sekta ya mitindo nchini (Vibrant Evaluation of Tanzania Fashion). Safari hii, kutakuwa na:Runway Mpya: Muonekano wa jukwaa la kisasa utakaopambwa na mavazi ya wabunifu wakali.Fashion Gurus: Uwepo wa wataalamu wa mitindo kutoka Afrika Kusini kuongeza ladha ya kimataifa na kutakuwepo na Tuzo za Heshima: Kutambua mchango wa Wabunifu (Designers), Wanamitindo (Models), Stylists, Wapiga picha, na Watu wenye ushawishi (Influencers).

Creative Director wa TFSA, Daxx Cruz, amewataka watanzania wote wapenda sanaa kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hili la kihistoria linalolenga kuishika mkono tasnia ya mitindo Tanzania.

"Twende tukawavike taji mastaa wa mitindo Tanzania. Let's shape the art of fashion TOGETHER!"

No comments