KOCHA Msaidizi wa timu ya Taifa ya
Vijana U-17, Bakari Shime amesema wamejipanga vyema katika harakati za kuwania
kufuzu fainalia za mataifa ya Afrika kwa vijana yanayotarajiwa kufanyika nchini
Madagasca.
Akizungumza na gazeti hili baada ya
mazoezi yaliyofanyika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, Shime amasema wanaendelea
na mazoezi katika uwanja wa Karume kwa wiki mbili kujiandaa na mchezo wa kwanza
dhidi ya timu ya Shelisheli.
“Mchezo wa kwanza wa kusaka tiketi
ya Madagascar tutacheza na Shelisheli hivyo tunajiandaa vyema kuhakikisha
tunafanya vizuri,” alisema Shime
Naye nahodha wa timu hiyo, Issa
Hajji amesema kila mchezaji anapambana kuhakikisha anabaki ndani ya timu hiyo
kutokana na mchujo unaoendelea hivyo ushindani ni mkubwa,” alisema Hajji.
Kwa sasa wachezaji waliopo kambini
ni 43 na watafanyiwa mchejo kubakiza 25 ambao wataiwakilisha nchini katika
kusaka kufuzu fainali za mataifa ya Afrika zitakazofanyika nchini Madagascar
2017.
No comments:
Post a Comment