SHIRIKISHO laSoka duniani (Fifa) limeikumbusha Simba kulipa deni wanalodaiwa na Donald Musoti.
Simba ilimtema beki huyo raia wa Kenya,Donald Musoti, ili ibaki na wachezaji watano wa kigeni kwa mujibu wa kanuni baada ya kumsajili Emanuel Okwi,lakini hata hivyo haikumlipa fedha zake za kuvunja mkataba.
Fifa iliwaandikia barua Simba kuhusu madai ya Musoti na kuwataka kumlipa mchezaji huyo stahiki zake,lakini uongozi wa Simba ukaweka ngumu wakidai hawawezi kumlipa wakati wao bado hawajalipwa fedha za mauzo ya Okwi kutoka Etoile.
Kwa hivi sasa suala la deni kati ya klabu ya Etoile ya Tunisia na Simba limekwisha baada ya Fifa kupata uthibitisho wa malipo hayo kiasi cha Dola laki tatu,na uongozi wa Simba wenyewe kuthibitisha pia kupokea kiasi hicho,hivyo Fifa wanaona hakuna sababu ya Simba kuendelea kukaa na deni la Donald Musoti.
Machi 19 mwaka huu,Simba wamepokea barua ya ukumbusho kutoka katika shirikisho hilo la soka duniani likikumbusha kuhusu malipo ya deni hilo la Musoti.
Mmoja wa viongozi wa Simba,amesema licha ya ukweli kwamba tayari wameshapokea kiasi hicho lakini kipaumbele chao cha kwanza siyo kulipa madeni isipokuwa ni kuzipeleka fedha hizo kwenye mradi wa ujenzi wa uwanja wao huko Bunju.
“Ni kweli tumepokea fedha tunazo zipo mikononi mwetu,lakini hatutalipa madeni kwa mtu yeyote isipokuwa hizi fedha tutazipeleka kuanza ujenzi wa kiwanja wa chetu kule Bunju,na wale wote wanaotudai kwa sasa watatusamehe tutawalipa kwa fedha nyingine huko mbele na siyo hizi za Okwi”
No comments:
Post a Comment