Saturday, March 26, 2016
MCHEZAJI WA TAIFA STARS ADI YUSSUF AANAYECHEZA ENGLAND AAHIDI FURAHA JUMATATU
MSHAMBULIAJI mpya wa timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’ Abdillahie Yussuf amefurahi kuitwa kuichezea nchi yake na kudai kufanya maajabu
Abdillahie ambaye anajulikana kama Adi anacheza Mansfield inayoshiriki ligi daraja la pili, Uingereza alisema yeye kama mtanzania amefurahi kuona anaungana na wachezaji wengine kuitumikia nchi yake na kuahidi kutoa ushirikiano.
“Nafurahi kuichezea nchi yangu hivyo sitawaangusha watanzania endapo nitapata nafasi ya kucheza ila joto linanipa shida kidogo lakini nitazoea,” alisema
Pia Adi alisema yeye ni raia wa Tanzania na alizaliwa Tanzania na baadae wazazi wake waliahamia Uingereza ambako ndiko alikokuliwa pia amefurahi kukutana na Mbwana Samatta mchezaji ambaye ameing’arisha Tanzania baada ya kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika
Naye Mshauri wa Ufundi wa benchi la ufundi la timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’Abdallah Kibadeni amesifu kiwango cha mshambuliaji huyo na kudai ataisaidia timu.
“Kwa muda mchache niliomwona nimeridhika na kiwango chake na naamini ataweza kuisaidia timu na nchi kwa ujumla,” alisema Kibadeni.
Adi ambaye anacheza namba tisa alizaliwa Februari 20, 1992 na alianza kucheza soka akiwa kwenye akademi ya Leicester City 2008-2011, 2011-2013 alicheza Burton Albion, 2013-2014 alikuwa Lincolin City na 2014 -2015 Oxford City.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment