Ray Wilkins ameiambia talkSPORT kuwa ni bora Chelsea na Eden Hazard wakatengana mwishoni mwa Msimu huu.
Msimu
uliopita Hazard aling’ara mno Chelsea, chini ya Jose Mourinho, ikitwaa
Ubingwa nay eye kupata Tuzo za Mchezaji Bora kadhaa lakini Msumu huu
amedorora mno kiasi cha kupotea kwenye ramani ya Wachezaji Bora. Jumatano, Hazard alianza Mechi ya Marudiano ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI na Chelsea kuchapwa 2-1 na PSG na kutupwa nje lakini Mashabiki wakamjia hasa baada ya kitendo chake cha kubadilishana Jezi na Mchezaji wa PSG Angel Di Maria wakati Timu zikitoka Uwanjani kwenda Mapumziko ya Haftaimu.
Sasa Wilkins, Staa wa zamani wa Chelsea na pia aliewahi kuwa Meneja Msaidizi wao, anaamini muda wa Hazrd kubakia Stamford Bridge umekwisha.Wilkins, ambae pia aliwahi kuwa Kepteni wa Timu ya Taifa ya England, amesema: “Katika Gemu chache zilizopita utaona moyo wake haupo tena Klabuni. Labda amevunjika moyo sijui. Lakini kuporomoka kwake kunashangaza. Ni bora aondoke Chelsea. Ni Mchezaji mzuri na kwenye Mechi na PSG kuna wakati alionyesha cheche zake lakini kama huna moyo na Timu kuna faida gani ubaki?”
No comments:
Post a Comment