YANGA imeleta
heshima kwa Watanzania baada ya leo kuifunga Cercle de Joachim ya Mauritius
katika mchezo wa maruadiano Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Kutokana na
matokeo hayo Yanga imefuzu hatua inayofuata kwa jumla ya mabao 3-0, baada ya
mchezo wa kwanza uliofanyika nchini Mauritius wiki mbili zilizopita Yanga
kushinda bao 1-0.
Ilikuwa
furaha kwa mashabiki wa Yanga walioingia jana kifua mbele ikiwa ni wiki moja
baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya watani zao Simba katika Ligi
Kuu Tanzania Bara.
Hata hivyo
Yanga licha ya ushindi huo, itabidi ijilaumu kutokana na kukosa nafasi nyingi
za wazi, ambazo zingewawezesha kupata ushindi mnono.
Lakini
washambuliaji wake wakiongozwa na Amis Tambwe, Simon Msuva, Malimi Busungu na
Paul Nonga kwa nyakati tofauti walishindwa kulenga lango la wapinzani wao.
Washambuliaji
hao kila walipokaribia lango la Yanga, ama walipiga michomo dhaifu iliyodakwa
na kipa au walipiga nje ya lango.
Yanga
ilianza kupata bao la mapema dakika ya tatu mfugaji akiwa Amiss Tambwe kutokana
na krosi ya Simon Msuva.
Bao hilo
liliwapa matumaini mashabiki wa Yanga kuona ushindi mnono, lakini kadri muda
ulivyokuwa unasonga mbele ndivyo matumaini hayo yalipokuwa yakififia.
Wageni
walijitahidi kupanga mashambulizi dakika za mwanzo kipindi cha pili, lakini
walijikuta wakipachikwa bao la pili dakika ya 56 mfungaji akiwa kiungo Thabani
Kamusoko kwa shuti lilitokana na mpira wa adhabu wa Juma Abdul.
Yanga
itakumbana na mshindi wa mchezo kati ya APR ya Rwanda na Mbabane Swallows ya
Swaziland.
No comments:
Post a Comment