Chama cha riadha kwa walemavu Tanzania (Tanzania Paralympic Committee [TPC]) kimepanga kushiriki katika mbio za Kilimanjaro Marathoni zinazodhaminiwa na kampuni ya GAPCO Tanzania wikiendi hii.
Akiongea
Dar Es Salaam, Bw. Peter Sarungi, ambaye ni Katibu Mkuu wa TPC, akitoa
shukrani zake kwa GAPCO, kampuni inayoongoza katika uuzaji wa mafuta
Tanzania kwa kudhamini mashindano ya Mbio za Kilimanjaro Marathoni za
KM10 kwa ajili kwa walemavu, zitawapa wanariadha walemavu nafasi si tu
nafasi ya kushindana miongoni mwao lakini pia kutangamana na wanariadha
kutoka sehemu mbalimbali duniani. “Tunaamini kwamba hii ni nafasi muhimu
kwa TPC ili kutambua wanariadha walemavu ambao wanaweza kuwakilisha
Tanzania kimataifa katika matukio mbalimbali ya kimichezo.
Alieleza
kwamba mashindano ya mbio za Kilimanjaro marathon za 10KM kwa walemavu
ambazo zinadhaminiwa na GAPCO ni shindano linalojumuisha baiskeli za
walemavu zenye matairi matatu zenye viwango vya kimataifa. Shinando
litafanyika tarehe 28 Februari 2016 sambamba na mbio za Kilimanjaro
Marathon Moshi, Kilimanjaro na usajili utaanza tarehe 26 Februari 2016.
“Mbio hizi ni kwa ajili ya walemavu wote wa Kitanzania, ambapo 60 kati
yao watakuwa wakidhaminiwa na GAPCO kushiriki kutoka Dar Es Salaam,
Arusha, Moshi na Zanzibar” aliongeza.
Tangu
GAPCO ilipoanza kudhamini Marathon mwaka 2011, wameshuhudia maendeleo
chanya mwaka hadi mwaka katika ubora wa mashindano. “ Tunashukurum
jitihada za GAPCO, si tu katika kufanikisha shindano hili kupitia
udhamini wake lakini zaidi ni kutoa msaada wa mahitaji maalumu kwa
washiriki wenye ulemavu katika mfumo wa chakula na usafiri.” alisema
MrSarungi. “Pia tunafuraha kuhusu kuongezeka kwa zawadi ya fedha taslimu
kwa mshindi ambapo ni Tsh. 1,000,000 kiasi hiki kinaweza kubadili
maisha ya washindi.
Bw.
Sarungi amewasihi watanzania kujitokeza kwa wingi kuwashangilia
wanariadha watakaoshiriki mbio hizi. “Tunataraji kushiriki na tunachukua
nafasi hii kuwakaribisha Watanzania kujitokeza na kuwapashangilia
wanariadha wetu katika tukio hili”.
Chama cha riadha kwa walemavu Tanzania (Tanzania Paralympic
Committee [TPC]) ni chama cha kitaifa na kimataifa kinachotambulika na
Serikali kupitia Baraza la Sanaa Tanzania na Chama cha ridhaa kwa
walemavu cha Kimataifa (International Paralympics Committee [IPC]). TPC
imekusudia kuwaleta pamoja wanariadha walemavu kutoka Tanzania kupitia
matawi ya kimikoa na kiwilaya na makundi mengine yenye hulka
zinazoshabihiana (shule za walemavu na timu za michezo).
No comments:
Post a Comment