Kuna
orodha ya wachezaji wengi ambao wanaweza kuwa wanamvutia kocha wa
Chelsea, Jose Mourinho lakini hakukosi mmoja ambaye ndiyo ambaye
anamkubali uwezo wake zaidi.
Akielezea
maisha yake ya ukufunzi nchini Singapore, Mourinho alimtaja mchezaji wa
zamani wa Chelsea, Frank Lampard kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya
Uingereza kwa muda wote ambao amefundisha soka Uingereza.
Alisema
ni ngumu kwake kumtaja mchezaji bora wa dunia sababu amefundisha
wachezaji mbalimbali na walio na viwango vikubwa lakini kwa kipindi
ambacho amekuwa akifundisha soka Uingereza Lampard ni bora zaidi.
Kocha Jose Mourinho akiwa na Frank Lampard
“Kwa
Chelsea kwa kipindi cha kwanza nilipofika nilikuwa na Frank Lampard
nadhani ndiyo mchezaji bora wa muda wote wa Lligi kuu ya Uingereza,”
Mourinho alikiambia kituo cha Straits Times.
“Nani ni mchezaji wangu bora? Ni ngumu kwangu kusema sababu nimefundisha baadhi ya wachezaji walio na viwango vya dunia,
“Nilienda
Inter (Milan), nilikuwa na (Zlatan) Ibrahimovic, nilikuwa na (Javier)
Zanetti,Madrid nilikuwa na (Cristiano) Ronaldo. Nikarudi Chelsea na
nikakutana tena na wachezaji wenye viwango vya dunia,” alisema Mourinho
na kuongeza.
“Kama
nimekutana na wachezaji wengi na walikuwa na uwezo mzuri sio vizuri
kusema huyu ni bora zaidi. Haiwezekani kushinda mataji mengi bila kuwa
na wachezaji ninawaheshimu wote”
No comments:
Post a Comment