Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, January 16, 2016

CANNAVARO AKERWA NA MKWASSA, AJIONDOA TAIFA STARS

Breaking News: Nadir Haroub astaafu kuchezea Stars 
Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na klabu ya soka ya  Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ameamua kustaafu kuichezea timu hiyo ili kuweka nguvu kwenye klabu yake Yanga.

Cannavaro amesema kwa sasa ana mambo mengi yanayomfanya ajiondoe kuichezea timu hiyo moja wapo ni kitendo kilichofanywa na kocha mkuu wa timu hiyo Charles Boniface Mkwassa kumteua mshambuliaji Mbwana Samatta kuwa nahodha bila kumpa taarifa kabla.

Jambo jingine Cannavaro amesema ni lawama anazopata kutoka kwa mashabiki ambao wanadai yeye ndiye anayeifungisha timu hiyo pale inapopata matokeo mabovu.

Cannavaro anasema maneno yamekuwa mengi na yalianza mara baada ya mechi ya marudiano ya kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia dhidi ya Algeria kule kwao.

“Katika mechi hiyo tulifungwa mabao 7-0, mechi hiyo muda mwingi tulijitahidi kupambana kuhakikisha tunawatoa Algeria lakini ikashindikana, cha ajabu mara baada ya mechi hiyo nilionekana mimi pekee ndiye niliyefungisha”, alisema Cannavaro.

Cannavaro kwa sasa ameamua kujiweka pembeni baada ya kocha mkuu wa Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa kumtangaza Samatta kama nahodha mpya.

Cannavaro amesema amepeleka barua rasmi kwa Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF ya kuwapa taarifa ya kustaafu kwake kuichezea timu ya taifa.

No comments:

Post a Comment