Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, November 16, 2015

STARS KUWAVAA ALGERIA LEO

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’  kilifanya mazoezi jana jioni saa 1 Algeria, sawa na saa 3 usiku kwa saa za Afrika Mashariki katika uwanja wa Mustapher Tchaker utakaotumika kwa mchezo wa leo dhidi ya wenyeji Algeria.
Stars inayonolewa na kocha mzalendo, Charles Boniface Mkwasa iliwasili salama juzi jioni katika mji wa Blida, uliopo takribani kilometa 75 kutoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Houari Boumediene jijini Algiers.
Mkwasa amesema mchezo wa kesho watajituma kadri ya uwezo kuhakikisha wanapata ushindi, makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa awali yamefanyiwa kazi na anaamini vijana wake watapambana kusaka ushindi katika mchezo huo.
Wachezaji wote 21 wapo katika hali nzuri, hakuna mchezaj majeruhi hata mmoja, hivyo kocha Mkwasa ana wigo mpana wa kumtumia mchezaji yoyote anayemuhitaji kwa ajili ya mchezo huo wa kesho.
Mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia nchini Urusi mwaka 2018, utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Mali na utaanza saa 1:15 usiku (Algeria) sawa na saa 3:15 usiku kwa saa nyumbani Tanzania na Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment