Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, November 19, 2015

SIMBA YALETA MCAMEROON KUCHUKUA NAFASI YA N'DAW, TAYARI YUKO DAR



Kiungo mshambuliaji Mcameroon Doumbia Ernest ametua nchini akipambana kupata nafasi ya kuziba pengo la Pape N’daw ambaye ametemwa rasmi.

Doumbia tayari yuko jijini Dar es Salaam na anatarajia kuanza mazoezi leo akijifua na Simba jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya majaribio na kama atafuzu, atasajiliwa wakati wa dirisha dogo.

"Kweli kuna mchezaji ambaye ataanza majaribio kesho (leo)," kilieleza chanzo.
Simba imeamua kumtema N’daw ambaye alifika nchini miezi mitatu iliyopita, lakini amekuwa hana msaada wowote na kikosi cha Dylan Kerr ambaye ndiye alimpendekeza kuja kujiunga na Simba.

Mchezaji mwingine ambaye Simba imemtema ni Mganda Simon Sserunkuma ambaye tayari yuko kwao nchini Uganda.

Kwa hisani ya Saleh jembe blog
 

No comments:

Post a Comment