Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, August 11, 2015

USAJILI WADIZI KUSOGEZWA MBELE



KLABU itakayochelewesha kuleta usajili wake itatozwa kiasi cha shilingi laki tano kwa kila mchezaji itakayemsajili mpaka Agosti 30.
Kauli hiyo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imekuja baada ya dirisha la usajili kusogezwa toka Agosti 6 hadi Septemba 20.
Akizungumza na wandishi wa habari, Afisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto alisema pia mwisho wa kufanya uhamisho wa kimataifa wa wachezaji kwa njia ya mtandao TMS ni Septemba 6.
“Kikao cha kamati ya sheria kitakaa Agosti 28 kwa ajili ya kuupitisha usajili na kitakaa tena Septemba 8 kwa ajili ya kupitisha usajili pia kuanzia Septemba 21- 27 itakuwa ni wiki ya pingamizi, ambapo majina yatabandikwa TFF Karume na kuwekwa kwenye mtandao ili kuwezesha vilabu vyenye pingamizi kuwawekea wachezaji mapingamizi”, alisema Kizuguto
Pia alisema Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inatarajiwa kuanza Septemba 12, 2015, Daraja la kwanza (FDL) inatarajiwa kuanza Septemba 17 na Ligi Daraja la pili inatarajiwa kuanza Oktoba 16 mwaka huu.
Wakati huo huo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema kuwa bado linaendelea na mazungumzo na wadhamini wa michuano ya Coca-Cola hivyo ratiba ya michuano hiyo itachelewa kutoka.
Hivyo, inawaomba kuwa na uvumilivu wakati mchakato wa mazungumzo hayo yanayokaribia ukingoni ukiendelea.

No comments:

Post a Comment