Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, August 11, 2015

TWIGA STARS KUCHEZA NA HARAMBEE STARLETS UWANJA WA AMAN ZANZIBAR



TIMU ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars), inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya Wanawake kutoka Kenya (Harambee Starlets) Agosti 23, 2015. 
Mchezo huo wa kirafiki utachezwa katika Uwanja wa Aman Kisiwani Zanzibar, ikiwa ni sehmu ya maandalizi ya kikosi hicho kujiandaa na fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) zitakazofayika nchini Congo-Brazzavile kuanzia Septemba 4 – 19, 2015.
Twiga Stars inaendelea na mazoezi kutwa mara mbili katika viwanja vya Aman na Fuoni chini ya kocha wake mkuu Rogasian Kaijage kujiandaa na fainali hizo za michezo ya Afrika, wachezaji wote waliopo kambini wapo katika hali nzuri wakiendelea kujifua na michezo ya Afrika.
Mechi hii imekuja wakati muafaka kwani tangu Twiga ianze safari ya kukata tiketi ya kucheza kushiriki fainali za michezo ya Afrika haijawahi kupata mechi yoyote ya kirafiki ya kimataifa.
Twiga imepangwa kundi moja na Nigeria, Ghana na wenyeji Congo Brazaville hivyo inahitaji ya maandalizi ya uhakika ili iweze kushiriki katika ushindani na siyo kuwa msindikizaji.

No comments:

Post a Comment