Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, August 11, 2015

TAIFA STARS YAANZA MAZOEZI BILA WACHEZAJI WA YANGA NA AZAM



TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeanza mazoezi katika Uwanja wa Karume kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2017 nchini Gabon.
Wachezaji wa Taifa Stars chini ya kocha wake mkuu Charles Mkwasa watakuwa wakijifua mara mbili kwa katika Uwanja wa Karume katika kujiweka sawa na maandalizi ya mchezo huo.
Kufuatia baadhi ya wachezaji kuwa na majukumu na timu zao kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Hisani utakaochezwa Agosti 22, Mkwasa amewaongeza wachezaji wengine kumi (10) kutoka katika orodha yake ya akiba.
Lengo la kambi hii ya awali ya siku tano, ni kupata nafasi ya kuwaona wachezaji katika mazoezi hayo kabla ya safari ya kuelekea nchini Uturuki Agosti 23 mwaka huu kwa kambi ya siku kumi.
Wachezaji walioitwa na kuanza mazoezi ni Said Mohamed, Vicent Andrew (Mtibwa Sugar), Mohamed Hussein, Ibrajim Ajibu (Simba SC), Hamis Ali, Juma Mbwana (KMKM), Tumba Sued (Coastal Unioni), Samuel Kamuntu (JKT Ruvu), Ibrahim Hilka (Zimamoto– Zanzibar) na Mohamed Yusuf (Prisons).
Wachezaji wengine waliopo kambini ni Said Ndemla, Hassan Isihaka, Abdi Banda(Simba SC), Rashid Mandawa (Mwadui FC), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Orgeness Mollel (Aspire Academy) na Abdulhaman Mbambi (Mafunzo).

No comments:

Post a Comment